Kocha Sir Alex Ferguson
|
Sir Ferguson alijiunga na
Manchester United tarehe 6 ya mwezi Novemba mwaka 1986 akirithi nafasi ya Ron
Atkinson na kwa kipindi hicho chote amefanikiwa kutwaa mataji 38 katika muda
huo wa miaka 27.
Mataji
ambayo ameshinda Sir Ferguson ni pamoja na mataji 13 ya Ligi Kuu nchini
Uingereza, makombe mawili ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, mataji
matano ya Kombe la Ligi pamoja na Makombe matano ya Chama cha Soka FA.
Sir Ferguson
mwenyewe amethibitisha uamuzi huo wa kujiuzulu wadhifa wake mwishoni mwa msimu
huu na kusema kwake huu ni muda muafaka kuchukua uamuzi kama huo na kukaa
pembeni.
Kocha huyo
mwenye heshima kubwa Old Trafford amesema ni muhimu kwake kuondoka sasa
kutokana na kufanikiwa kujenga kikosi madhubuti ambacho kimefanikiwa kutwaa
taji msimu huu mapema.
Sir Ferguson
amekiri anajivunia vilivyo kuwa na kikosi imara ambacho kinawachezaji wenye
wastani mzuri wa umri ambao wanaweza wakaisadia Manchester United kwa kipindi
kirefu zaidi.
Kocha huyo
mwenye msimamo madhubuti amesema anaondoka Old Trafford akiwa amechangia
kuifanya timu hiyo kuwa na vifaa vyenye kiwango cha hali ya juu kwa timu kama
Manchester United.
Sir Alex
Ferguson ametangaza kustaafu kuifundisha Manchester United baada ya miaka 27
ndani ya Old Trafford.
|
Sir Ferguson
ametoa kauli hiyo baada ya kumaliza muda wa mazoezi asubuhi hii na kueleza
anatoa shukurani za dhati kwa familia yake kwa ushirikiano waliokuwa wanampa
kipindi chote na hasa mkewe Cathy.
Kocha huyo
amesema kwa sasa anaangalia kuanza majukumu ya kuwa Mkurugenzi na Balozi wa
Manchester United ili kuhakikisha anaendelea kuisaidia timu hiyo kupata
mafanikio zaidi katika siku za usoni.
Mrithi wa
Sir Ferguson ameanza kutajwa kuwa Kocha wa Everton David Moyes ambaye anamaliza
muda wake wa kuinoa timu hiyo huku akiwa bado hajasaini mkataba mpya wa
kuendelea kusalia Goodison Park.
Makocha
wengine wanaotajwa kurithi nafasi ya Sir Ferguson ni pamoja na Jose Mourinho
anayekinoa kikosi cha Real Madrid pamoja na Jurgen Klopp ambaye amepata
mafanikio makubwa akiwa Borussia Dortmund.
Jupp
Heynckes
|
David Moyes
|
Carlo
Ancelotti
|
Ole Gunnar
Solkjear
|
Mourinho au
Jurgen Klopp
|
No comments:
Post a Comment