Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
amefanya uteuzi wa Mabalozi Wapya kujaza nafasi zilizo wazi na kuanzisha Ofisi
za Ubalozi nchini Uholanzi na Comoro. Aidha Mheshimiwa Rais amefanya uhamisho
wa Balozi kutoka kwenye kituo kimoja.
Mabalozi
wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:-
Bw.
Wilson M. K. Masilingi;Ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Bw.
Masilingi ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa,
Arusha, (AICC) na aliwahi kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kati ya mwaka 1995 – 2010. Aidha, katika kipindi cha mwaka 1998 – 2005
alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya Utawala
Bora.
Bw.
Chabaka Faraji Ali Kilumanga, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro.
Hadi uteuzi huu unafanyika, Bw. Kilumanga alikuwa Balozi Mdogo katika ofisi ya
Ubalozi nchini Uingereza.
Bw.
Modest Jonathan Mero, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja
wa Mataifa, Geneva. Kabla ya uteuzi Bw. Mero alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje
Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, New
York.
Kadhalika,
Mheshimiwa Rais amemhamisha Balozi Philip Sang’ka Marmo kutoka Ubalozi wa
Jamhuri ya Watu wa China na kwenda Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.
(John
M. Haule)
KATIBU
MKUU,
WIZARA
YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
12
MEI, 2013.
No comments:
Post a Comment