Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeahirishwa tena jioni hii baada ya Mbunge
wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA) kukataa kuomba radhi.
![]() |
Naibu
Spika Ndugai.
|
Marekebisho
ya hotuba ya upinzani kuhusu CUF na ushoga haya hapa Mabadiliko katika ukurasa wa 8 aya ya pili inayoanza
na maneno ‘Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa chama cha CUF....na kuishia na
maneno…Israel Liberal ‘ sasa isomeke: “Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama
cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali chama hicho ni
mwanachama wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali Duniani (Liberal International).
Kwa
mujibu wa tovuti ya umoja huo CUF imejiunga na Oxford Congress ya Liberal
International Mwaka 1997.
Mwaka
huo huo Liberal International ilitoa msimamo wa pamoja wa umoja huo uliotwa
Liberal Manifesto (Ilani ya Kiliberali) ya 1997 iliyopitishwa katika mkutano
mkuu wake wa 48 uliofanyika tarehe 27 mpaka 30 Novemba 1997 katika ukumbi wa
Mji wa Oxford nchini Uingereza.
Katika
ilani hiyo ya waliberali, umoja wa vyama hivyo ulikubaliana msimamo wa pamoja,
nanukuu: “the extension of the rules of equality to sexual minorities and the
recognition that homesexuality and lesbianism are legitimate expressions of
personal proclivities”. Kwa Tafsiri rahisi waliberali hao walipitisha ajenda ya
waliberali katika karne ya 21 (The Liberal Agenda in the 21st Century) ya
kuutambua ushoga na usagaji kama matendo halali.
Hii
ni kwa mujibu wa tangazo la Umoja huo kwenye mtandao wao wa waliberali
ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn
Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(Liberalism)
kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu
mmoja mmoja.
Kupitia
umoja hao CUF inashirikiana na vyama vingine kama vile LPC ya Canada, Det
Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal………” Ezekiah
Dibogo Wenje Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa 30 Mei 2013.
No comments:
Post a Comment