Taarifa za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima
anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord (May 03,2013) iliyopo Kariakoo
Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni
kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.
Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka
chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina
mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye
alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro,
nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na
siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo
kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.
Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na
kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na
kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.
Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo
pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.
Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.
Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na
taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika.
Blog hii inatoa pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo.
No comments:
Post a Comment