Baada ya Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kutoa Wosia wake sasa Meneja na Mume wa Mwanamuziki huyo Gadan G Habash azungumza haya kuhusu kauli ya Mkewe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 04, 2013

Baada ya Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kutoa Wosia wake sasa Meneja na Mume wa Mwanamuziki huyo Gadan G Habash azungumza haya kuhusu kauli ya Mkewe.



Gada G Habash.
Leo nilipata nafasi ya kuzungumza na Gadan G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake,kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC FM haya ndio yalikuwa majibu ya maswali aliyomuuliza Gada G Habash.

 



Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?




Gadna G: Ni maneno ambayo yametoka moyoni mwake na ni maneno mbayo anajitetea kama msanii, mimi kama Meneja ukiacha pia kama mke wangu naendelea kumsapoti kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsapoti na kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba watu wasifikirie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana na experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.



Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati ila hakusema, lakini siku za hivi karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.





Hii ni kama vita mmejipangaje..?





Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie na ukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama, lakini ulikuwepo tayari kwa hiyo watu wanajua kwa sasa, kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanamfumo dume wa kufanya kazi na alipoachana nao aliona kama wanamfuatilia kulekule ambapo yeye alipo.





Nini mlikiona kama chokochoko...?





Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia akaona kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufuata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye glasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.





Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?





Lady Jay Dee
Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategemea umma wa Watanzania au hata mashabiki kwa ujumla, kwa kuwepo kwake.



Jay Dee anapata sapoti nzuri kutoka kwa Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yakeee. Yani lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.





Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?





Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhuru, kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaweza ukasababishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa. Wangeogopa leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....





Kauli yako ya mwisho ni ipi..?




Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na kusikia ukweli ili kama wanakosea wasiendelee kukosea wabadilikee….

Mwisho..!



AKIONGEA NA MTANGAZAJI DAN CHIBO MTANGAZAJI WA TBC FM,NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA.



 CHINI -Wosia wake  Judith Wambura ‘Lady Jaydee’





Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.


Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.


Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige mame,Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.


Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai,Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.


Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.


Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.


Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.


Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..


Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.


Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.


Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??


Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.


Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.


Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??Roho gani hiyo??


Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu.


JIDE.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad