Serikali
imesema hali ya lishe nchini hairidhishi na kwamba asilimia 42 ya watoto walio
na umri chini ya miaka mitano wamedumaa, asilimia 16 wana uzito pungufu wakati
asilimia tano wamekonda.
Aidha,
asilimia 11 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa yaani miaka 15 hadi 49
wamekonda wakati asilimia 58 ya wajawazito wana upungufu wa damu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi,
Peniel Lyimo, alisema hali hiyo inapunguza kasi ya Taifa ya maendeleo.
Alisema
kutokana na hali hiyo, Rais Jakaya Kikwete atazindua kampeni maalumu ya kuweka
virutubishi kwenye mafuta ya kula, unga wa mahindi na unga wa ngano, ili jamii
yote iweze kupata lishe muhimu.
Alisema
tatizo la utapiamlo linaendelea kuongezeka na linaathiri zaidi wakazi wa
vijijini na kwamba linachangia kuwepo magonjwa yasiyoambukiza kama ya moyo,
kisukari na saratani.
Kaimu
Katibu Mkuu Kiongozi
na
Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu),
Peniel Lyimo.
|
Lyimo ambaye
pia ni Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu), alisema tatizo la lishe linaanza
tangu mtoto anapokuwa tumboni hadi siku 1,000 za mwanzo baada ya kuzaliwa na
kwamba utapiamlo unaathiri ukuaji wa mtoto kiakili na kimwili; madhara ambayo
hayawezi kurekebishwa.
Hata hivyo,
alisema serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuanzisha madawati ya lishe
kwenye Halmashauri zote nchini na mkakati wa sasa wa kuongeza virutubishi
kwenye unga na mafuta ya kula.
Alisema Rais
Kikwete atazindua kampeni hiyo ya kitaifa Mei 16 mwaka huu, katika viwanja vya
Mnazi Mmoja baada ya kufanya ziara kwenye viwanda vinavyozalisha mafuta na unga
Mei 15.
Wakati huo
huo, Mshauri wa Rais wa Masula ya Lishe, Dk. Wilibrod Lorri, alitaja mikoa
inayoongoza kwa utapiamlo kuwa ni Kagera, Mbeya, Kigoma, Iringa, Arusha, Lindi,
Shinyanga, Tanga, Morogoro, Manyara, Mtwara, Rukwa, Ruvuma na Dodoma.
Mingine ni
Singida, Mwanza, Pwani, Tabora, Pwani, Mara, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba.
No comments:
Post a Comment