Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyoundwa chini ya Sheria ya Chakula Dawa
na Vipodozi Sura ya 219, ili kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa,
vipodozi, na vifaa tiba kwa lengo la kulinda afya ya jamii dhidi ya madhara
yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo.
Ili kutimiza wajibu huo, TFDA inasimamia pamoja na mambo mengine udhibiti wa uingizaji wa vyakula kutoka nje ya nchi na utengenezaji wa vyakula ndani ya nchi kwa ajili ya kulinda afya za watumiaji. Katika udhibiti wa vyakula hivyo, michakato mbalimbali hufanywa ili kuwa na uhakika juu ya usalama wake kwa; kufanya tathmini na uchunguzi wa kimaabara, kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa usalama wa bidhaa kwenye soko na hatimaye kusajili majengo na vyakula baada ya kujiridhisha juu ya usalama wake.

Kutokana na mfumo wa udhibiti uliopo, Mamlaka imesajili bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyofungashwa ikiwa ni pamoja na vinywaji aina ya soda zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje.
Hivi karibuni kulitolewa taarifa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kueleza kuwa kinywaji cha soda ni sumu.
Mamlaka ina mashaka juu ya taarifa iliyotolewa
kwa sababu haidhani kama ilitolewa kwa kuzingatia misingi ya kisayansi. TFDA
inapenda kuwatoa hofu watumiaji wa kinywaji hiki kuwa, soda ni bidhaa ya
chakula ambayo inatumika kote duniani na huzalishwa kwa kuzingatia viwango vya
ubora na usalama.
Kwa upande wa TFDA, soda zote zilizosajiliwa zimepitia katika
mchakato ambao unatoa uhakika juu ya usalama wake kwa lengo la kulinda afya ya
binadamu.
Tunapenda kutoa rai kwa vyombo vya habari kufanya utafiti wa kina hususan katika masuala yanayohusu ushahidi wa kisayansi ili kuondoa uwezekano wa kutoa taarifa kwa umma ambazo zinaweza kujenga hofu na mashaka ambayo hayastahili.
Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kupitia;
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
Barabara ya Mandela, Mabibo External,
S.L.P 77150,
Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2450512/2450751/2452108
Fax: +255 22 2450793
Barua pepe: info@tfda.or.tz
No comments:
Post a Comment