Tafiti
nyingi duniani zimegundua kuwapo na msukumo na mhemko wa tamaa za ngono kwa
wanaume.
Majibu kadha wa kadha ya tafiti hizo yamekuwa yakitoa majibu sawa,
ikiwemo suala la maumbile ya mwanamume na namna anavyompokea mwanamke yoyote
machoni pake.
“Rafiki
yangu wa karibu niliyempokea na kumtafutia kazi nchini Marekani alinisaliti kwa
kutembea na mume wangu,” anaanza kwa kusema Christina Edward (34) (siyo jina
lake kamili) Mtanzania anayeishi katika Jimbo la Houston Texas nchini Marekani.
Christina
anasema haikumuwia rahisi kung’amua tukio hilo la aibu, mpaka alipotonywa na
jirani yake ambaye hakuwa na ukaribu naye. “Jirani yangu aliwaona, akanipa
taarifa za usaliti huo.
Nilifuatilia kwa muda mrefu na kuwakuta wakiwa katika
flat (nyumba) anayoishi rafiki yangu huyo iliniuma sana, mpaka leo siwezi sahau
tukio lile japo miezi kadhaa imepita sasa nahisi aibu kila wakati,” Huyu ni
mmoja kati ya mamilioni ya wanawake duniani wanaokumbana na adha za namna hii.
Mwananchi liliwafanyia mahojiano baadhi ya wanasaikolojia ambao walithibitisha
kuwapo na ukubwa wa tatizo hilo hapa nchini, wakilinganisha kesi wanazozipokea
zinazohusiana na usaliti wa waume na wake waliopo ndani ya ndoa.
Kauli
ya wataalamu
wa saikolojia.
Mwanasaikolojia
na Mkurugenzi wa Kliniki ya NEHOTA inayotoa huduma ya ushauri iliyopo Makongo
Juu jijini, Dk Bonaventura Balige anasema japo tafiti kadhaa zimefanyika,
lakini Tanzania hakuna utafiti uliofanyika mpaka sasa, ila anakubaliana na
tafiti za nje kulingana na kesi anazozipokea na uzoefu wake katika maisha ya
kawaida.
“Nakubaliana
na tafiti zilizowahi kufanyika nje, kituo changu kimepokea kesi kadhaa kama
hizo na zifananazo na hizo. Mara nyingi tunapopokea kesi huwashauri kwanza
kutafuta chanzo cha tatizo. Stress (msongo wa mawazo) ndiyo huwa chanzo cha
wanaume walio wengi kujikuta wakiingia katika vitendo hivyo.”
Anasema
msongo wa mawazo kwa wanaume husababishwa na vitu vingi, ikiwamo kazini, mtaani
au nyumbani kwake, mwanamke asipokuwa makini hujikuta familia yake ikiwa
mashakani.
Dk
Balige anasema amepokea kesi zaidi ya tatu zilizohusu mume kuwa na uhusiano ya
kimapenzi na rafiki wa mkewe, lakini pia amepokea kesi zaidi ya nne za waume
kutembea na wafanyakazi wa ndani wa kike wake zao wakiwa kazini.
Hata
hivyo amewahi kupokea kesi kadhaa za wake kutembea na rafiki za waume zao. huku
lukuki zikiwa ni usaliti katika ndoa.
“Licha
ya kuumbwa hivyo mwanamume huyu ana uwezo wa kupenda mwanamke mmoja tu, ila
kinachomfanya awe na wanawake wengi ni tamaa.
Wapo
wanaoweza kudhibiti tamaa zao, lakini wengine ni vigumu. Dk Balige anasema kuwa
mwanamume akishindwa kuhimili mhemko wa mwili wake, huwa chanzo cha kuharibu
uchumi wa familia na mwishowe huishia kutelekeza familia “wanawake nao
wanatumia udhaifu wa wanaume katika kuchuma pesa, hivyo mwanamume asipoweza
kuzisimamia hisia zake hujikuta akitelekeza familia,” anasema.
Mwanasaikolojia
Jaykesh Rathid mwenye asili ya Asia aliyefungua ofisi inayotoa huduma ya
ushauri maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam anasema, wanaume wana kawaida
ya kutongoza wanawake waliowazoea wakiwamo rafiki za wake zao kwa kuwa huwawia
rahisi wakati wa kujieleza. “Mara chache sana mwanamume kutongoza mwanamke
anayekutana naye kwa mara ya kwanza.
Waume
wengi hawana kawaida hiyo hasa waliooa, kwanza hufikiria mtu anayetongoza
hamfahamu kiundani huenda anaweza kuwa ndugu au mtu wa karibu na mkewe, huona
afadhali kwa mtu anayemjua au anayefanya naye kazi ofisi moja,” anasema
Jaykesh.
Jaykesh anasema kiashiria huwa sababu ya kwanza kwa mtu kufanya
kitendo hicho “kabla rafiki wa mke hajafanya kosa hilo, mara nyingi mwanamume
au yeye mwanamke huonyesha ishara ya kumpenda mhusika, na kwa kuwa anafahamu
baadhi ya mambo kupitia kwa mkewe, humwia rahisi kujua mbinu zipi atumie
kumpata,” anasema.
Anasema
mwanamume ameumbwa na tamaa “Hii isipothibitiwa na mke mwanamume atatoka nje,
kesi nyingi napokea hapa ni watu wa karibu, inaweza kuwa rafiki wa mke,
msichana wa kazi za ndani au mtu anayefanya naye ofisini au maeneo mengine ya
kazi.”
Kisa
na mkasa halisi
kilichowahi kutokea.
Kisa
cha Christina, Mtanzania aliyeolewa na raia wa Marekani kilitokana na kumpa
uhuru rafiki yake aliyemwamini kuwa anaweza kuwa mlinzi mzuri katika nyumba
yake kwa kipindi anachotafuta kazi, huku yeye akifanya kazi shifti ya usiku.
“Nilimlipia
nauli ya ndege kutoka Tanzania baada ya miezi mitatu alifanikiwa kupata chuo na
kazi. Mbadala wake alihama harakaharaka. Mawasiliano yalikuwa ya mbali mpaka
nilipopata taarifa kuwa ananichukulia mume.”
Chanzo:Mwananchi.







No comments:
Post a Comment