![]() |
| Bungeni Dodoma. |
Safari
hii utoro huo unawahusisha mawaziri na siyo wabunge.
Tukio kama
hilo liliwahi kutokea Julai 22, mwaka jana wakati wa mjadala wa Bajeti wa
Wizara hiyo kiasi cha kufanya moja ya vikao vyake kuahirishwa kutokana na utoro
wa wabunge.
Kufuatia
utoro huo, Mbunge wa Mwibala CCM KANGI LUGORA ameomba muongozo wa Spika juu ya
kitendo hicho anachodai kuwanyima haki wananchi.
Akiomba mwongozo huo LUGORA amesema, licha ya Wizara hiyo kuwa na masuala yanayomgusa moja kwa moja mwananchi wa chini ambaye ni mkulima, mahudhurio ya mawaziri hayaridhishi huku akikiomba kiti kuhairisha kujadiliwa kwa bajeti hiyo.
| Job Ndugai. |
Hata hivyo baadhi ya Wabunge wakichangia bajeti hiyo akiwemo SELEMANI BUNGARA na JOHN CHEYO wameitaka Serikali kuurekebisha mfumo wa Stakabadhi ghalani kwani badala ya kuwa mkombozi umeendelea kuwadidimiza wakulima kiuchumi.
![]() |
| Utoro Bungeni. |
Julai 22
mwaka jana, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia alisimama kuomba mwongozo wa
Naibu Spika, Job Ndugai kutokana na Bunge kutokuwa na nusu ya wabunge wote
kinyume cha Kanuni ya Bunge wakati wa Bajeti ya Wizara hiyo ya Kilimo, Chakula
na Ushirika.
“Idadi ya wabunge wote ni 352 lakini wabunge waliomo humu ndani haizidi 110, ambapo nusu ya wabunge wote ni 176 hivyo kuendelea kupitisha bajeti hiyo ni kuvunja kanuni,” alisema Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
Baada ya kujiridhisha kwamba idadi hiyo ilikuwa ndogo, Naibu Spika aliahirisha kupitishwa kwa Bajeti hiyo.
Bajeti
hiyo ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imehitimishwa leo tayari kwa
Bajeti ya Wizara ya Maji kuanza kujadiliwa hapo kesho.







No comments:
Post a Comment