Ile ripoti
maarufu kuliko zote, ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (RIPOTI
YA CAG), imetinga rasmi bungeni asubuhi hii, na kwa mujibu wa sheria mpya ya
CAG iliyopitishwa mwaka jana, ilibidi na serikali kuwasilisha majibu ya hoja za
CAG sambamba na taarifa hiyo ya CAG, kitu ambacho serikali haikufanya.
Mbunge wa
Bariadi, Mhe. John Memosa Cheyo, amesimama kuomba muongozo wa spika, serikali
inapovunja sheria siku ya kwanza ambayo ilitakiwa ianze kutekelezwa!. Spika
akaomba majibu kwa waziri na mwanasheria mkuu, wote hawakuwa na majibu!,
amewapa mpaka mchana serikali ilete majibu!.
Kwa
msiokumbuka, ni RIPOTI YA CAG ya mwaka jana, ilileta songombwingo na patashika
ya mashati kuchanika kule bungeni Dodoma kwa serikali kuponea chupu chupu
kuvunjwa kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Spika
akaikingia kifua, na JK akakubali matokeo kwa kulivunjilia mbali baraza la
mawaziri, na kuwatosa mawaziri wenye makandokando yaliyoichafua serikali ya JK,
hivyo kuunda baraza jipya ambalo sasa ni la serikali safi!, na kama itaendelea
kwa usafi huu, kutakuwa na haja kweli ya kuibadili seririkali mwaka 2015?.
Kwa
wafuatiliaji makini, ripoti hizi zinapatikana online kwenye website ya NAOT
National
Audit Office of Tanzania
Financial Year 2011/2012 11 Apr 2013
- Local Government Authorities Report 2011/2012 6248 kB
- Central Government Report 2011/2012 1970 kB
- Public Authorities and Other Bodies 2011/2012 1464 kB
- Performance and Forensic Report 2011/2012 1121 kB
- Donar Funded Projects Reports 2011/2012 3134 kB
Mwaka wa Fedha 2011/2012 11 Apr 2013






No comments:
Post a Comment