![]() |
| Profesa John Nkoma |
Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa watu watakaobanikia kuvunja
Sheria ya Mawasiliano ya Electroniki na Posta (EPOCA) ya 2010, kwa kushindwa
kutimiza vipengele vya sheria hiyo vinavyozuia matumizi na taratibu mbaya za
uuzaji na usajili wa namba za simu za mkononi.
Licha ya
onyo hilo, mamlaka hiyo imewakumbusha wananchi baadhi ya makosa ambayo
hufanyika katika taratibu za uuzaji, utumiaji na usajili wa namba ili
wajiepushe na rungu kali litakalowakuta.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma kwenye taarifa yake kwa umma jana, iliwataka
wananchi kufahamu makosa ambayo hukiuka vipengele vya sheria ya Epoca 2010
katika matumizi na biashara ya namba za simu za mkononi.
Baadhi ya
makosa yaliorodheshwa, ni kuuza au kusambaza namba ya simu bila kibali cha mtoa
huduma za simu ambaye ana leseni kutoka TCRA; kutumia namba ya simu ambayo
haikusajiliwa na kutoa taarifa ya uongo au maelezo yasiyo sahihi wakati wa
usajili.
Mengine ni
kuchakachua simu ya mkononi au namba na kutoandikisha taarifa zake husika kabla
ya kuitoa au kuiuza.
Profesa
Nkoma aliwakumbusha watoa huduma wote na wakala wao kuhakikisha wanazingatia
kuweka kumbukumbu na taarifa kuhusu wakala wao na kuandikisha watumiaji
wanaonunua, au kupatiwa namba za simu.
“Kutotoa
taarifa za wateja bila idhini ya mamlaka husika na wauzaji wote waliodhinishwa
wana wajibu,” alisema Profesa Nkoma.






No comments:
Post a Comment