![]() |
| Rais Uhuru Kenyatta |
Aidha mpaka sasa bado wizara
mbili hazijapewa viongozi.
Uteuzi
uliotangazwa leo unatimiza idadi ya mawaziri 16 kati ya 18 ambao wataunda
baraza la kwanza la mawaziri tangu kuchaguliwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa
awamu ya nne ya Jamhuri ya Kenya .
Wanasiasa wa
muda mrefu Charity Ngilu na Najib Balala wamo kwenye orodha iliyotangazwa leo.
Ngilu
ataiongoza wizara ya ardhi huku Balala akielekea katika wizara ya madini na
migodi.
Michael
Kamau ndiye waziri mpya wa usafirishaji wakati mtaalamu wa maswala ya uchumi, Phyllis
Chepkoskey Kandie akipewa wizara ya
utalii.
David
Chirchir amekabidhiwa wizara ya nishati na mafuta.
![]() |
| Rais Kenyatta na Bw.Ruto. |
na Baraza jipya
limezusha maswali juu ya namna wengi wa mawaziri walioteuliwa wanavyotoka
katika makabila ya Kikuyu na Kalenjin, ya Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake
William Ruto.
Akijibu maswali
ya waandishi wa habari juu ya wasiwasi huo, Rais Kenyatta amesema wamejaribu
kuweka uwakilishi wa majimbo yote ya nchi kwa kadri ya uwezo wao. ''Kwa bahati
mabaya baraza hili sio kubwa kama yale yaliyotangulia,'' alisema Kenyatta.
Jumanne wiki
hii, Rais Kenyatta alikuwa ameteua waziri wa fedha, waziri wa mambo ya nchi za
nje, waziri wa habari na waziri wa afya.
Wizara
ambazo bado zinasubiri kujua watakaoziongoza ni ile ya utumishi, usalama wa
kijamii na huduma kwa umma, pamoja na wizara ya mambo ya ndani na tawala za
majimbo.
Amina
Mohamed ni miongoni mwa mawaziri wapya, anayeongoza wizara ya mambo ya nje na Maswali
yamekuwa yakiulizwa kuhusu sababu ya kulitangaza baraza la mawaziri hatua kwa
hatua.
Mchambuzi wa
masuala ya kisiasa kutoka Kenya Bobby Mkangi, ameiambia DW kuwa changamoto
kubwa inatokana na utekelezwaji wa makubaliano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na
makamu wake William Ruto, ambayo yanasema vyama vyao vitagawana madaraka nusu
kwa nusu.
Kabla ya
kupitishwa rasmi, mawaziri wateule watachunguzwa na kamati ya bunge,
inayowajumuisha maspika wa bunge na seneti pamoja na wabunge kutoka mabaraza
hayo mawili.
Hata hivyo,
muungano wa kisiasa wa Jubilee wa Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake unao wingi
wa wabunge katika mabaraza hayo.
![]() |
|
President
Uhuru Kenyatta Congratulates Ambassador Raychelle Awour Omamo after naming her
as the nominnee for the post of Cabinet Secretary in the Ministry of Defence at
State House Nairobi.
|
![]() |
|
Mr.Najib
Balala after naming him as the nominee for the post of Cabinet Secretary in the
Ministry of Mining.
|
![]() |
|
President
Uhuru Kenyatta Congratulates Anne Waiguru after naming her as the nominee for
the post of Cabinet Secretary in the Ministry of Devolution and Planning at
State House Nairobi.
|
![]() |
|
President
Uhuru Kenyatta Congratulates Dr Hassan Wario Arero after naming him as a nominee
for the post of Cabinet Secretary in the Ministry of Sports, Culture and Arts
at State House Nairobi.
|
![]() |
|
Mr Adan
Abdulla Mohamed the nominee for the post Cabinet Secretary of Industrialization
and Enterprise Development.
|
![]() |
|
Mr Davis
Chirchir after naming him as the nominnee for the post of Cabinet Secretary in the
Ministry of Energy and Petroleum at State House Nairobi.
|
![]() |
|
President
Uhuru Kenyatta Congratulates Prof. Jacob Kaimenyi after naming him as the
nominee for the post of Cabinet Secretary in the Ministry of Education at State
House Nairobi.
|
![]() |
|
Mr James
Wainaina Macharia, the nominee for the post of Cabinet Secretary in the
Ministry of Health.
|
![]() |
|
Presdent
Uhuru Kenyatta with Deputy President William Ruto introducing the new Cabinet
Secretary nominee in the Ministry of Foreign Affairs Amb. Amina Mohamed to
Kenyans at State House Nairobi.
|
![]() |
|
Introducing
Dr Fred Okengo Matiangi as the nominee for the post of Cabinet Secretary in the
Ministry of Information Communication and Technology (ICT) at State House
Nairobi.
|
![]() |
|
Rais
Kenyatta Introducing Mr Henry K. Rotich as the nominee for the post of Cabinet
Secretary in the National Treasury at State House Nairobi.
|
























No comments:
Post a Comment