Habari ndiyo hiyo:- Yanga Bingwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2012/2013 na taji lao la 24 tangu watwae kwa mara ya kwanza mwaka 1968. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 27, 2013

Habari ndiyo hiyo:- Yanga Bingwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2012/2013 na taji lao la 24 tangu watwae kwa mara ya kwanza mwaka 1968.


Timu ya Yanga SC  ya Dar es Salaam imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu  soka Vodacom Tanzania bra leo (April 26,2013) , kufuatia sare ya goli 1-1 katika mchezo wa ligi hiyo baina ya wenyeji Coastal Union na Azam FC ya Dar es Salaam,kwenye  Uwanja wa Mkwakwani, Tanga leo.



Matokeo hayo yanamaanisha, Azam FC waliokuwa washindani wakuu wa Yanga SC yenye pointi 56, hawawezi tena kufikisha pointi hizo ambazo wanazo mabingwa hao wapya, kwani hata wakishinda mechi zao nyingine  mbili zilizobaki, watamaliza na pointi 54. 



Mchezaji aliyepeleka shangwe na vigelegele Jangwani leo ni Danny Lyanga, ambaye aliifungia Coastal bao la kusawazisha dakika ya 72 ya mchezo huo. 



Azam FC
Azam FC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo wa leo, lililofungwa na beki Aggrey Morris kwa penalti dakika ya 60, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Gaudence Mwaikimba kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari  na beki Yussuf Chuma- na refa Andrew Shamba wa Pwani akaamuru pigo hilo.


Matokeo haya yanakuwa sawa na Coastal kulipa fadhila kwa Yanga, kwani hata wao, ubingwa wao pekee wa Ligi Kuu waliochukua mwaka 1988 ulitokana na ‘msaada’ wa wana Jangwani huo.




ORODHA MABINGWA WA JUMLA LIGI KUU.


1965 : Sunderland (Dar es Salaam)

1966 : Sunderland (Dar es Salaam)

1967 : Cosmopolitans (Dar es Salaam)

1968 : Yanga

1969 : Yanga

1970 : Yanga

1971 : Yanga

1972 : Yanga

1973 : Simba

1974 : Yanga

1975 : Mseto SC (Morogoro)

1976 : Simba

1977 : Simba

1978 : Simba

1979 : Simba

1980 : Simba

1981 : Yanga

1982 : Pan African

1983 : Yanga

1984 : Simba

1985 : Yanga

1986 : Tukuyu Stars (Mbeya)

1987 : Yanga

1988 : Coastal Union (Dar es Salaam)

1989 : Yanga

1990 : Simba 

1991 : Yanga

1992 : Yanga

1993 : Yanga

1994 : Simba

1995 : Simba

1996 : Yanga

1997 : Yanga

1998 : Yanga

1999 : Mtibwa Sugar (Morogoro)

2000 : Mtibwa Sugar (Morogoro) 

2001 : Simba

2002 : Yanga

2003 : Simba

2004 : Simba

2005 : Yanga

2006 : Yanga

2007 : Simba (Ligi Ndogo)

2008 : Yanga

2009:  Yanga 

2010: Simba SC

2011: Yanga SC

2012: Simba SC

2013: Yanga SC
 
Msimu huo, mshindani wa Coastal katika mbio za ubingwa alikuwa Simba SC ambaye ili kutwaa taji hilo, alihitaji kushinda mechi ya mwisho dhidi ya African Sports mjini Tanga huku akiomba Wagosi wa Kaya walale mbele ya Yanga Uwanja wa Taifa.



Yanga
Lakini Yanga wakacheza ‘kichovu’ na Athumani China akaenda kupiga penalti ‘kiviivu’ akakosa, Coastal ikishinda 2-0 na kusherehekea taji pekee la ubingwa wa Ligi Kuu, licha ya Simba pia kushinda 3-0 dhidi ya Sports Tanga. 



Hili linakuwa taji la 24 kwa Yanga, tangu watwae kwa mara ya kwanza mwaka 1968.


Aidha, huu unakuwa msimu wa pili mfululizo, Azam wanaukosakosa ubingwa wa Ligi Kuu, baada ya msimu uliopita pia kuzidiwa kete na Simba SC. 

 

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts raia wa Uholanzi,  ni kati ya makocha wanaopewa nafasi ya kuwania nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu Sredojevich Milutin ‘Micho’ kufukuzwa kazi.



Micho raia wa Serbia aliyewahi kuwa kocha wa Yanga alitupiwa virago baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwa miezi minne mfululizo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad