PICHA:Jerome Onesmo (53) amekutwa amekufa kandokando ya barabara iendayo mgodi wa uchimbaji madini ya Nickel kata ya Bugarama wilaya ya Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 08, 2013

PICHA:Jerome Onesmo (53) amekutwa amekufa kandokando ya barabara iendayo mgodi wa uchimbaji madini ya Nickel kata ya Bugarama wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Jerome Onesmo (53) amekutwa amekufa kandokando ya barabara iendayo mgodi wa uchimbaji madini ya Nickel kata ya Bugarama  wilaya ya  Ngara mkoani Kagera(Picha na Shaban Ndyamukama).

Mtu huyo  aliyetambuliwa kwa jina la Jerome Onesmo (53) amekutwa amekufa kandokando ya barabara iendayo mgodi wa uchimbaji madini ya Nickel kata ya Bugarama  wilaya ya  Ngara mkoani Kagera.




Afisa mtendaji wa kijiji cha Rwinyana kata ya Bugarama wilayani Ngara Bw Venace John amesema mtu huyo  aliondoka  nyumbani kwake April 6 saa 11 jioni kwenda kusaga mahindi na alikutwa njiani kesho yake akiwa amefariki dunia.




Akizungumza na wanahabari mtoto  wa pili wa marehemu Nuwaka Pambano (32) alisema baba yake alikuwa amekunywa pombe kupita kiasi na alipokuwa njiani kwenda kusaga ambapo alikuwa akianguka hovyo na alipowekwa kando kando ya barabara  aliahidi kunyanyuka na hadi pale alipokutwa amepoteza maisha.




Aidha mtoto mkubwa wa marehemu Sibomana Jerome 35 akiwa katika eneo la tukio alikokutwa baba yake akiwa amefariki dunia , aliwashangaza wananchi waliofika kushuhudia mwili wa marehemu pembeni mwa barabara kwa kujivua nguo  na kujitosa kwenye madimbwi ya maji machafu.




Kijana huyo aliwatuhumu wananchi kuwa baba yake amefariki kwa kupewa sumu na ndugu zake wanaogombania mashamba yanayotarajiwa kutolewa fidia na mradi wa uchimbaji madini aina ya Nickel kijiji humo.




Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philipo Karangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi wilayani Ngara linafanya uchunguzi kujua chanzo cha kifo cha mwananchi huyo.

mtoto mkubwa wa marehemu Sibomana Jerome 35 akiwa katika eneo la tukio alikokutwa baba yake akiwa amefariki dunia.(Picha na Shaban Ndyamukama)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad