![]() |
| Godbles Lema |
Baada ya
Mbunge huyo kuachiliwa huru, umati wa wanachama wa Chadema waliokuwa wamejazana
katika Mahakama hiyo walifanya maandamano makubwa kwenda katika Ofisi za Chama
hicho zilizopo maeneo ya Ngarenaro.
Mbunge huyo
amekutwa na makosa matatu ambapo kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo
cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki
hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa
kupiganiwa.
Kosa la pili
ni pale alipotamka kuwa “Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na
mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye
send-off.
Kosa la tatu
ni pale alipotamka kwa wanafunzi kuwa “Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi
hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa hatakuja hapa kama
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili
mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya
jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia
inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala
bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za
binadamu’’.






No comments:
Post a Comment