Mabomu yaliyolenga Mbio za Marathon huko Boston Marekani huenda yalifichwa ndani ya sufuria za kupikia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 17, 2013

Mabomu yaliyolenga Mbio za Marathon huko Boston Marekani huenda yalifichwa ndani ya sufuria za kupikia.


Mabomu yaliyolenga Mbio za Marathon huko Boston Marekani huenda yalifichwa ndani ya sufuria za kupikia. Hii ni kwa mujibu wa majasusi.Baadhi ya picha zilizochapishwa kwenye taarifa ya shirika la ujasusi-FBI zinaonyesha vipande vipande vya chuma.



Shambulio hilo la Jumatatu wiki hii liliwaua watu saba na kuwajeruhi wengine zaidi ya 170. Miongoni mwa walipoteza maisha ni pamoja na mvulana wa miaka minane na mwammke wa miaka 29, pamoja na mwanafunzi raia wa China.



Huku haya yakiarifiwa Rais Barack Obama anatarajiwa kuzuru Boston hapo Alhamisi kwa maombi maalum ya kuomboleza vifo hivyo.Obama pia atawahutubia waathiriwa na jamaa zao.


Mwandishi wa BBC mjini Boston anasema mkesha wa maombi kwa waathirka ulifanyika hapo Jumanne, huku wenyeji wakitafakari sababu za kutaka kulenga mbio hizo ambazo huwa kivutio cha wengi.


Madaktari wanaowahudumia majeruhi wamesema bomu hilo lilikua na vyuma, na vipande vya makombora. Majeruhi kadhaa wamekatwa miguu na mikono.

Chanzo:BBC SWAHILI



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad