Kampuni ya usafirishaji ya Sultani Salim ya jijini Dar es Salaam,imeanza ujenzi wa nyumba ya Bi.Bibiana John mkazi wa Kumuyange wilayani Ngara, ambayo iligongwa na kubomolewa na gari la kampuni hiyo katika ajali iliyotokea siku ya Jumamosi jumaa lililopita. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 16, 2013

Kampuni ya usafirishaji ya Sultani Salim ya jijini Dar es Salaam,imeanza ujenzi wa nyumba ya Bi.Bibiana John mkazi wa Kumuyange wilayani Ngara, ambayo iligongwa na kubomolewa na gari la kampuni hiyo katika ajali iliyotokea siku ya Jumamosi jumaa lililopita.



Kampuni ya usafirishaji ya Sultani Salim ya jijini Dar es Salaam,imeanza ujenzi wa nyumba ya Bi.Bibiana  John mkazi wa Kumuyange wilayani Ngara mkoani  Kagera, ambayo iligongwa na kubomolewa na gari la kampuni hiyo katika ajali iliyotokea siku ya Jumamosi(April 13,2013) jumaa lililopita.

Wakala wa Kampuni hiyo Bw.Martin Raphael ameiambia Redio Kwizera FM kuwa tayari maandalizi ya ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya Mhanga huyo na familia yake umeanza.




Bw. Rafael amesema kuwa pamoja na shughuli ya ujenzi wa nyumba hiyo, kampuni hiyo pia imeshiriki kufanya mazishi ya watu wawili waliopoteza maisha katika ajali hiyo.




Amesema kuwa kampuni hiyo imetoa rambi rambi ya shilingi laki moja kwa kila familia na kuongeza kuwa kampuni hiyo itatoa fidia ya piki piki iliyogongwa katika ajali hiyo  baada ya kupata taarifa ya mkaguzi wa polisi  kitengo cha usalama barabarani.




Aidha watu wawili walifariki dunia  papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari  hilo aina ya Mercedec benz lenye namba ya usajili T 908 ABZ semitrailer lililokuwa ikitokea nchini Burundi, kuacha njia (April 13,2013) muda wa saa 12 jioni na kupinduka katika eneo la Kumuyange nje kidogo ya mji wa Ngara mkoani Kagera.




Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wilaya ya Ngara  Abel Mtagwa aliwataja watu hao waliofarki katika ajali hiyo kuwa ni Edward Filimon alie kuwa akiendesha pikipiki yake yenye namba za usajiri T 756 BZJ na abiria wake ambae hadi sasa haja fahamika jina lake.


Kamanda Mtagwa aliwataja majeruhi wa ajari hiyo kuwa ni Dereva wa gari hilo Hajji Omary Ibrahim(29) mkazi wa gongolamboto jijini Dar es salaam  ambaye amaruhusiwa baada ya kutibiwa na tingo wake aliyejulikana kwa jina la Kambi simba(40) ambaye bado anaendelea kupata matibabu katika Hospital ya Murugwanza wilayani Ngara mkoani Kagera.




Aidha chanzo cha ajari hiyo ni  gari hilo kufeli  mfumo wa Breki  jambo ambalo Dereva wake alishindwa kulimudu kuliendesha ndipo lilipanda mtaro na kubomoa nyumba hiyo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad