![]() |
|
Kutoka kushoto: Halima Mdee, Ester Bulaya na Neema Hamid.
|
Baadhi ya Wabunge
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walihudhuria mafunzo ya
kijeshi katika kambi tofauti za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), walipata msoto wa
nguvu.
![]() |
|
Baadhi
ya wabunge wakiwa
katika
pozi na wanajeshi
wengine.
|
Tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa kwamba wabunge hao wangepewa mafunzo
kwa kubembelezwa kutokana na nafasi zao, walikutana na msoto wa nguvu mwanzo
hadi mwisho.
Kuonesha
jinsi ambavyo msoto ulikuwa wa nguvu, katika kambi ya Tanga, siku tu ya
utambulisho, mbunge wa Chadema (jina tunalo), alizimia.
Vilevile,
kwenye Kambi namba 832, Ruvu, Pwani, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine,
alishindwa kuhimili kishindo cha depo, hivyo akatoroka, japo mafunzo yenyewe
yalikuwa ya muda wa wiki tatu tu.
ILIKUWA KAZI
KWELI
Siku ya
kwanza tu ya kuripoti kambini, wabunge wote walipigwa vipara na baada ya hapo,
ilifuata awamu ya kupima afya.
“Jeshi ni jeshi
tu, tulipimwa ukimwi bila hata kuandaliwa wala kupewa ushauri,” alisema mmoja
wa wabunge waliohudhuria depo hiyo (jina tunalo) kisha akaongeza: “Mfano mimi
ningeambiwa kule kuna kupima ukimwi hata nisingeenda, nilikuwa sijapima kama
miaka saba, dah kule ni hatari.”
![]() |
|
Mbunge wa
Kawe (Chadema), Halima Mdee, akinyolewa nywele.
|
KUHUSU
VIPARA
Mbunge
mwingine alisema: “Walichotuweza ni ile tunaripoti tu, tunanyolewa vipara
halafu ndiyo taratibu nyingine zinafuata. Kama wangekuwa wanatuonesha picha ya
kile kitakachofanyika kabla ya kutunyoa, wengi wetu tungetimka mapema.
“Tatizo
unanyolewa halafu ndiyo unapelekwa kupimwa ukimwi, sasa ukikataa kupima na una
kipara chako, mtaani utarudi vipi? Hata kunyoa, wengine tuliingia na rasta,
lakini wakatupiga upara wa wembe harakaharaka bila hata kungoja kuzifumua.”
MAFUNZO YANA
FAIDA?
![]() |
|
...Wakiwa
mazoezini.
|
Mbunge wa
Viti Maalum kwa tiketi ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Mara, Ester Bulaya,
alisema kuwa anashukuru kupata mafunzo ya kijeshi, kwani yamemjenga kwa kiasi
kikubwa.
“Japo ni
kazi lakini tunatamani muda uongezwe, maana wiki tatu zilikuwa fupi, program ni
nyingi, kwa hiyo tukatakiwa kufanya kwa pamoja,” alisema Bulaya kisha
akaongeza: “Imenijenga kweli, najiona mkakamavu mwenye uwezo zaidi wa kutumikia
wananchi.”
Kwa upande
wa Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, alisema: “Natamani kila mtu awe
anapitia mafunzo ya JKT, maana siyo tu yanakujenga kiukakamavu, bali pia
yanakupa uzalendo na ari ya kuwatumikia wananchi.”










No comments:
Post a Comment