VIDEO: Bw Uhuru Kenyatta apishwa rasmi kuwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Kenya na kuwataka wananchi wa taifa hilo kuungana pamoja ili kuchochea maendeleo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 10, 2013

VIDEO: Bw Uhuru Kenyatta apishwa rasmi kuwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Kenya na kuwataka wananchi wa taifa hilo kuungana pamoja ili kuchochea maendeleo.



Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Bw. Uhuru Kenyatta akiwapungia maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo (April 09,2013) kwenye sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Kasarani,jijini Nairobi Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete,Mabalozi na watu wengine mbalimbali.


Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Bw. Uhuru Kenyatta akisoma hotuba yake mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika ndani ya uwanja wa Kasarani,Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais wa nchi mbalimbali.

Rais Uhuru Kenyatta akila kiapo cha Urais,kuwa rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofana kwa kiasi kikubwa ndani ya uwanja wa kasalani.

Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Makamu wake William Ruto.


Bw. Uhuru Kenyatta amewataka wananchi wa taifa hilo kuunganisha mawazo yao kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili ili kuchochea maendeleo.




Akitoa hatuba yake ya kwanza  baada ya kuapishwa katika uwanja wa Kasarani mjini Nairobi kwa ajili ya kuanza rasmi majukumu yake na makamu wake Bw.William Ruto,Rais Kenyatta amesema kuwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi ulioupa ushindi muungano wa Jubilee, kila Mkenya anapaswa kulitumikia taifa lake kwa nafasi yake ili kuharakisha maendeleo.





Aidha amewataka wapinzani wake katika uchaguzi uliopita kuungana naye kufanya kazi kwa ajili ya Wakenya ili kuboresha hali za maisha ya wananchi wao na kwamba hatapuuza ushauri kutoka kwa kiongozi yeyote waliyechuana naye katika uchaguzi huo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad