Cardinal Jorge Mario Bergoglio, 76, from Argentina was announced as the Catholic Church's new pope Wednesday night - Name: Pope Francis - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 13, 2013

Cardinal Jorge Mario Bergoglio, 76, from Argentina was announced as the Catholic Church's new pope Wednesday night - Name: Pope Francis

Cardinal Jorge Mario Bergoglio
Hatimae Kanisa katoliki limemchagua Cardinal Jorge Mario Bergoglio, miaka 76, kutoka Nchini  Argentina kuwa Baba Mtakatifu Mpya ambaye Atachukuwa  Wadhifa wa Upapa kufuatia  Papa Benedict wa 16 aliyejiuzuli.


Papa Mpya alichaguliwa katika duru ya tano ya upigaji kura uliofanywa na makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika kanisa la Sistine Chapel huko Vatican ,Jijini  Roma.

 

Kwa wakati huu mbali na maelfu ya watu waliokusanyika eneo la St. Peters huko Vatican jina la Papa mpya ,atakuwa ni Baba Mtakatifu Francis.



Bergoglio will become the first pope from Latin America. He won the necessary two-thirds vote after only two days of the conclave. Several other candidates were considered front runners, including Cardinal Peter Kodwo Appiah Turkson, who would have become the first African pope in modern times.



Kadinali Jorge Mario Bergoglio
Ni Kadinali Jorge Mario Bergoglio   Amezaliwa December 17, 1936 (age 76), Buenos Aires Nchini Argentina.



Ni padre wa shirika la Majesuit akipata elimu yake katika chuo kikuu cha Buenos Aires
Kabla ya kuchaguliwa leo kua Papa alikua askofu mkuu wa Buenos Aires tangu mwaka 1998 na mwaka 2001 aliteuliwa kua Kadinali na Papa John Paul II.



Ni papa wa Kwanza kutoka bara ambalo lina aminika kua na waumini wengi wa Kanisa Katoliki (Latin America) akichagua jina la Francis I akifata mfano wa Mtakatifu Francis wa Asis mwanzilishi wa shirika la watawa wakapuchini.



Papa Francis amechaguliwa kufatia kujiuzulu wadhifa wa upapa kwa aliyekua Mtangulizi wake Papa Benedict XVI ambapo habari zinasema kua Papa huyu alishika nafasi ya Pili mwaka 2005 wakati Papa Benedict alipochaguliwa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad