![]() |
The Windsor
Atlantica
|
Kikosi cha
timu ya taifa ya Uingereza kimepanga kula maisha Rio de Janeiro wakati wa
michuano ya Kombe la Dunia 2014, kwa kuweka kambi yake kwenye hoteli ya The
Windsor Atlantica, inayojulika iliyopo kwenye fukwe za Copacabana.
Vijana hao wa kocha
Roy Hodgson wataishi kwenye hoteli hiyo ya nyota tano, ambayo iko pembezoni mwa
bahari, wakati wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Brazil kwenye uwanja wa
Maracana, Juni 2, mwaka huu.
![]() |
Eneo la Beach:
Hoteli ya England (Jengo refu zaid) ikiangalia fukwe za Copacabana
|
![]() |
The Windsor
Atlantica yatakuwa makazi ya Uingereza, mwanzoni wa Juni.
|
![]() |
Ndani
ya hoteli hiyo
ambayo
Timu ya Taifa ya
Uingereza
watafikia
|
Wamedhamiria
kutumia hoteli hiyo hiyo wakati wa michuano ya Kombe la Dunia, mwaka mmoja
baadaye, iwapo kikosi hicho kitafuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka
2014.
Jengo la
hoteli hiyo ya nyota tano ndilo refu zaidi kwenye eneo lilipo, huku likiangalia
fukwe za Copacabana .
Moja ya
maeneo ya kuvuti Kaskazini mwa Havana: Aidha Timu hiyo ya Taifa ya Uingereza watakula bata kwenye moja ya
maeneo mazuri zaidi ya Rio.
Hoteli hiyo
ina vyumba 54 huku Uingereza wakitarajiwa kuishi kwenye ghorofa ya pili na ya
tatu ya hoteli hiyo ambapo wakiwa hapo
watakuwa na sehemu yao maalumu ya kula, matibabu na kujiachia.
Lakini
watakutana na wananchi wengi pale watakapokatiza kwenye eneo la mapokezi la
hoteli hiyo.
Haitafanana
na makao makuu yao ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini ambaklo
walikaa kwenye hoteli ya Royal Bafokeng Sports Campus iliyopo Rustenburg,
hoteli ambayo iliwakera baadhi ya wachezaji.
Hoteli hiyo
inasehemu ya spa na bafu linye shower saba kwa ajili ya kupunguza uchovu.
Windsor
Atlantica pia wanatoa mataulo ya ufukweni, viti na miamvuli.
Kwenye
michuano ya Euro mwaka jana nchini Poland, Uingereza waliweka makazi yao
katikati ya mji wa Krakow.
Lakini
hoteli ya Stary ilichaguliwa mahususi kwenye michuano hiyo kwa sababu za
kiusalama kwa sababu kulikuwa na walinzi waliohakikisha wachezaji wanapata muda
binafsi.
Wakati
wakiwa hawana kazi jijini Rio, Uingereza watakuwa wakipumzika kwenye fukwe kubwa zaidi
duniani za Copacabana.
Na kwa jambo
lolote ambalo England watakuwa wanataka kukabiliana nalo juu ya masuala ya
Kombe la Dunia, Uongozi wa FIFA utakuwa jirani yao kwenye hoteli ya Copacabana
Palace.
No comments:
Post a Comment