Wachezaji 22 wa Taifa Starz waitwa kambini Januari 6 ,2013 jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 01, 2013

Wachezaji 22 wa Taifa Starz waitwa kambini Januari 6 ,2013 jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.


Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka huu.


Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam.


Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).



Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).



Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).



Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).




Aidha pia  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua ofisa wake Leslie Liunda wa Tanzania kwenda Ethiopia kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa utoaji leseni kwa klabu zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.



Ofisa huyo atawasili nchini Ethiopia kesho (Januari 2 mwaka huu) ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 6 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.



Utekelezaji wa kazi yake hiyo nchini Ethiopia utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), Wizara ya Michezo ya nchi hiyo, viongozi wa klabu na mameneja wa viwanja husika.



Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad