Mustafa Mkulo. |
Wakati
baadhi wakiugulia kwa machungu hayo, kwa upande mwingine lipo kundi la wale
wanaosherehekea neema iliyowajia mwaka huohuo, baada ya nyota zao kung’ara
kisiasa na kujikuta wakikwaa nafasi za uongozi, pengine ambazo hawakuzitarajia.
Miongoni mwa
matukio yaliyowatikisa wanasiasa ni hatua ya Rais Jakaya Kikwete kupangua
Baraza la Mawaziri, kutenguliwa kwa baadhi ya matokeo ya chaguzi za wabunge na
uchaguzi wa ndani wa CCM ambao uliwaweka kando baadhi ya vigogo wa chama hicho.
Godbless Lema |
Kadhalika,
yapo matukio yenye sura ya kipekee ambayo yanawagusa wanasiasa kama Godbless
Lema ambaye alianguka kisiasa kwa ubunge wake kutenguliwa na Mahakama Kuu,
Kanda ya Arusha mwanzoni mwa mwaka jana, lakini akaibuka tena shujaa baada ya
kurejeshewa nafasi hiyo na Mahakama ya Rufani, Desemba 2012.
Tukio kubwa
ambalo lilitikisa siasa za Tanzania ni lile la mabadiliko katika Baraza la
Mawaziri ambayo yaliwaweka kando mawaziri sita ambao walikuwa wakiziongoza
wizara nyeti zinazosimamia rasilimali za nchi na huduma za afya na uchukuzi.
Waliong’olewa
ni Mustafa Mkulo (Fedha), William Ngeleja (Nishati na Madini), Ezekiel Maige
(Maliasili na Utalii), Omari Nundu (Uchukuzi), Dk Cyril Chami (Viwanda na
Biashara) Dk Haji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii). Pia panga hilo liliwakumba
waliokuwa Naibu Mawaziri, Dk Lucy Nkya (Afya na Ustawi wa Jamii) na Dk Athuman
Mfutakamba (Uchukuzi).
William Ngeleja. |
Kuanguka kwa
Mkulo, Ngeleja na Maige kulitokana na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) iliyozihusisha wizara zao na ufisadi. Dk Mponda na Dk
Nkya, waling’olewa kutokana shinikizo la madaktari ambao walifanya mgomo
uliotikisa sekta ya afya nchini.
Kwa upande
wake, Nundu naibu wake, Dk Mfutakamba waling’olewa kutokana na kashfa ya ujenzi
wa gati bandarini ambao uliwagawa kiasi cha kutofautiana bungeni, wakati Dk
Chami naye aliponzwa na ugomvi na aliyekuwa naibu wake, Lazaro Nyalandu. Hata
hivyo Nyalandu alipona baada ya kuhamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Tanzania. |
Walioula.
Mabadiliko
hayo yalikuwa neema kwa wateule wapya wakiwamo wale ambao hawakuwahi kuwa
wanasiasa kama ilivyo kwa Profesa Sospeter Muhongo ambaye aliteuliwa kuwa
Waziri wa Nishati na Madini.
Profesa
Muhongo alipewa naibu wawili; George Simbachawene (Nishati) na Stephen Masele
(Madini) ambao walikuwa wabunge.
Wabunge
wengine walioula ni Dk William Ngimwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na
kupewa naibu wawili ambao nao hawakuwa katika duru za kisiasa; Saada Mkuya
Salum na Janeth Mbene.
Na wakati huohuo ambao Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi,
James Mbatia aliteuliwa na Rais kuwa mbunge.
http://www.mwananchi.co.tz/habari.
No comments:
Post a Comment