Mazishi ya msanii wa filamu nchini, Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' yatafanyika siku ya Ijumaa, Januari 4 mwaka huu katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 02, 2013

Mazishi ya msanii wa filamu nchini, Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' yatafanyika siku ya Ijumaa, Januari 4 mwaka huu katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.


Marehemu Sadick Juma Kilowoko
'Sajuki' enzi za uhai wake
.
Mazishi ya msanii wa filamu nchini, Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' yatafanyika siku ya Ijumaa, Januari 4 mwaka huu katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.


 

Taarifa ambazo zimeridhiwa na maamuzi ya familia na ndugu wa karibu pia zimetoka kwa msemaji wa Bongo Movie na wahusika wa maandalizi ya mazishi hayo, wanasema ndugu wa Sajuki wameridhia marehemu kuzikwa hapa na sio Songea kama wengine wanavyotangaza.Kuhusu kusogeza mpaka ijumaa, msemaji huyo akasema, ni kutokana na kusubiri ndugu wa marehemu wanaotoka sehemu mbali mbali kuja Dar es salaam kwa ajili ya mazishi hayo, wengi wakitokea Songea.
Marehemu Sadick Juma Kilowoko
'Sajuki' enzi za uhai wake
 akiwa na mkewe Wastara Juma.

Sajuki ambae alifariki usiku wa kuamkia tarehe 2 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipata matibabu, atazikwa siku ya ijumaa ya tarehe 4 katika makaburi ya Kisutu, ambapo mazishi hayo yataanza muda wa saa 5 asubuhi.Marehemu Sajuki amefariki leo alfajiri Marehemu Sajuki alizaliwa mwaka 1986 mkoani Ruvuma na ameacha mke na mtoto mmoja wa kike.


YAH: SALAAM ZA RAMBIRAMBI.
Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii wa tasnia ya filamu nchini Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki.
Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Sajuki ambaye mchango wake unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Tunaomba mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.Imetolewa na


Ghonche materego

Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la Taifa.


Hii ni clip niliyoichukua Hotel Arusha wakati Marehemu Sajuki akiwa amepumzishwa baada yakudondoka stejini na kesho yake akapelekwa Dar kuendelea na matibabu. Hapo chumbani kulikuwa wasanii wa watu waliokuja kwenye show yake, utaweza kumuona msanii Roma pamoja na Kala Jeremiah na Yusuph Mlela.
Mungu ailaze roho ya marehemu Juma Kilowoko (Sajuki) mahala pema peponi, Amen.

Post Bottom Ad