![]() |
Moja ya Kundi la ng’ombe |
Mkuu
wa Wilaya ya Ngara,Bw. Costantine Kanyasu ametoa agizo hilo pamoja na kupiga
marufuku viongozi wa vijiji wilayani humo kuwapatia ardhi wahamiaji wenye
mifugo kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza
na wafugaji wakubwa na wadogo wa Kata za Kasulo na Rusumo pamoja na viongozi wa
kata hizo, Mkuu huyo wa wilaya amesema tamko hilo limetolewa baada ya kuwepo kwa
baadhi ya wafugaji wenye asili ya Kinyarwanda na wengine kutoka wilaya za mikoa
ya hapa nchini wanaoingia wilayani Ngara na ng’ombe wengi na kuwanyanyasa wazalendo
wenye ng’ombe wachache.
Bw.Kanyasu
amesema ili kuhakikisha amani na utulivu vinapatikana ndani ya siku 30,
viongozi wa vijiji kwa kata zote wilayani Ngara wafanye usajili upya wa
kuwatambua wafugaji wageni toka nje ya vijiji vyao na mifugo waliyo nayo na
kubaini walioingia kihalali na walioingia kinyume, ili sheria iweze kuchukua
mkondo wake.
Amesema
serikali inafanya kazi ya kulinda na kutetea haki za wananchi na sio kutetea
kundi dogo lenye uwezo wa kifedha na kuwanyanyasa wachache, kwani kufanya hivyo
ni kukiuka haki za binadamu na kukwepa uwajibikaji kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment