Msanii Omari Omari aliyefariki Januari 8,2013 afajiri atazikwa Januari 9, 2013 Dar es salaam saa 7 mchana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 09, 2013

Msanii Omari Omari aliyefariki Januari 8,2013 afajiri atazikwa Januari 9, 2013 Dar es salaam saa 7 mchana.

Marehemu Omari Omari
Msanii nyota wa miondoko ya Mchiriku, Omari Omari, aliyefariki Januari 8,2013 afajiri atazikwa January 9, 2013 Dar es salaam saa 7 mchana.


Marehemu Omari Omari aliugua kwa muda mrefu ambapo hata siku chache zilizopita alishindwa kumaliza show yake aliyokua nayo Mbagala, alipanda kwenye stage na kuimba wimbo mmoja tu baada ya hapo akashuka na kuanza kutapika.



Omari Omari aliyetamba na wimbo “Kupata Majaaliwa” ndani yake kukiwa na mstari mkali unaosema ndefu amekosa ng’ombe lakini mbuzi kapewa, alifariki katika hospitali kuu ya Temeke baada ya kuugua ugonjwa wa kifua kikuu. Msiba uko Temeke Mikoroshini nyumbani kwa baba yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad