![]() | |
Bw. Issa Ngumba. |
Taarifa
kutoka Jeshi la Polisi wilayani Kakonko zinasema kuwa Bw Ngumba amepotea tangu
January 05 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mke wake Bi. Rukia
Yunus kuwa anakwendwa Muhange senta wilayani Kakonko na kwamba hajarudi
nyumbani hadi sasa.
Kufuatia
tukio hilo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Muhange
wanaendelea kumtafuta katika mapori ya kijiji hicho baada ya rafiki zake
kueleza kuwa aliwaanga kuwa anakwenda kutafuta dawa msituni.
![]() |
Bw. Issa Ngumba. |
Aidha jeshi
la polisi Wilayani Kibondo limeomba kampuni za mitandao ya simu anayotumia Bw
Ngumba kusaidia kutambua simu zake zilipotumika kwa mara ya mwisho ili
kurahisisha upatikanaji wake.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Mke wa Bw Issa Ngumba, Bi Rukia Yunus amesema kuwa wananchi
walio wengi ambao walikuwa wakimtafuta maporini wamerudi kijiji hapo baada ya
kumkosa.
Habari:Radio Kwizera
Habari:Radio Kwizera
Ameshapatikana akiwa amekufa na mazishi ni leo tar 8 Jan 2013 - Tuapdatie usiwe mzee wa analojia.
ReplyDeleteAsante kwa hilo..tayari ndugu na ndo tumetoka mazikoni Kakonko na tunarudi Ngara.
ReplyDelete