…. Mungu ailaze roho ya marehemu Issa Ngumba…… mahala pema peponi, Amen…alikuwa ni Mwandishi wa habari Radio Kwizera FM wilayani Kakonko,auwawa na Watu wasiofahamika, amezikwa leo (Januari 08,2013)nyumbani kwake katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 08, 2013

…. Mungu ailaze roho ya marehemu Issa Ngumba…… mahala pema peponi, Amen…alikuwa ni Mwandishi wa habari Radio Kwizera FM wilayani Kakonko,auwawa na Watu wasiofahamika, amezikwa leo (Januari 08,2013)nyumbani kwake katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko.

Marehemu Issa Ngumba
Aliyekuwa mwandishi wa habari wa Redio Kwizera FM  katika wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Bw Issa Ngumba aliyeuwawa na watu wasiofahamika baada ya kutoweka tangu Januari tano mwaka huu amezikwa leo (Januari 08,2013)nyumbani kwake katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko.


Akiongea baada ya Mazishi, Mwenyekiti wa Halmsahuri ya wilaya ya Kibondo Bw Juma Maganga amesema kifo cha Ngumba ni pigo kwa wilaya na taifa kwa ujumla.



Mkuu wa kituo cha Polisi Muhange OSC Alex Zakaria amesema Jeshi la Polisi litahakikisha waliofanya mauaji ya Mwandishi huyo wa Habari wanakamatwa na  wanafikishwa katika vyombo vya sheria.



Aidha Mwili wa Issa Ngumba umeonekana leo (Januari 08,2013)majira ya saa tatu na nusu Asubuhi karibu na mlima Kudyaluheta katika kijiji cha Muhange ukiwa umenyongwa. 



Marehemu Issa Ngumba
Kwa mujibu wa Dr Primus Ijuma wa Kituo cha Afya Kakonko aliyefanya uchunguzi wa mwili huo amesema umeonyesha Bw Issa Ngumba ameuawa kwa kunyongwa na kisha kupigwa risasi katika mkono wake wa kushoto.



Aidha Simu na pesa alizokuwa nazo Bw Issa Ngumba hazikuchukuliwa lakini pia watu waliofanya tukio hilo waliacha bastola karibu na mwili wake.



Awali taarifa za Jeshi la Polisi zilisema kuwa Bw Ngumba alipotea tangu January 05 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mke wake Bi. Rukia Yunus kuwa anakwendwa Muhange senta wilayani Kakonko na hakuonekana tena hadi alipokutwa porini amefariki.





Katika Salamu zake za rambi rambi Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Kigoma (KGPC) kimeeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwandishi huyo.




Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Kigoma Bw Deogratius Nsokolo amelaani mauaji hayo na kulitaka Jeshi la Polisi mkoani Kigoma kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha mauwaji hayo  .
 



…. Mungu ailaze roho ya marehemu  Issa Ngumba…… mahala pema peponi, Amen.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad