![]() |
Wilaya ya Kibondo |
Mkuu wa JKT,
Meja Jenerali Raphael Mahuga alisema katika taarifa yake jana kuwa wanafunzi
hao watatakiwa kujiunga na jeshi hilo ifikapo Machi 2, mwaka huu.
Shule hizo
za sekondari ni Kibondo, Musoma, Kibaha, Ilboru, Bagamoyo, Jitegemee, Tabora
Wavulana, Nganza, Mtwara Wasichana, Ihungo, Kilakala, Benjamin Mkapa, Maswa
Wasichana, Dodoma, Tumain-Singida, Galanos, Ashira, Nangwa-Manyara, Iyunga,
Mpanda, Lindi, Iringa Wasichana, Kawawa-Iringa na Ruhuwiko-Songea.
Taarifa hiyo
ilisema maofisa wa JKT watakwenda kwenye shule hizo kuanzia Januari 9, mwaka
huu kwa ajili ya kutoa utaratibu wa mafunzo na kambi ambazo watakwenda.
“Mkuu wa JKT
kwa mamlaka aliyopewa kisheria ya mwaka 1964 na kufanyiwa mapitio mwaka 2002,
chini ya kifungu cha sheria namba 5,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa
“Anawaita vijana watakaohitimu kidato cha sita mwaka 2013 kujiunga na JKT kwa
mujibu wa sheria ifikapo terehe 2, Machi 2013.”
Utaratibu wa
mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ulisimamishwa tangu mwaka 1994.
Akiwasilisha
bajeti ya Wizara ya Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Julai mwaka
jana, Waziri wake, Shamshi Vuai Nahodha
alisema kambi zilizopo za JKT zina uwezo wa kuchukua vijana 20,000 kwa wakati
mmoja, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka huu wataanza kwa majaribio na
vijana 5,000.
Alisema
wanafunzi 41,348 wanatarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha sita katika mwaka
2013 na kwamba vilikuwa vikiandaliwa vigezo ili kuwapata vijana 5,000 ili
kujiunga na JKT.
Kwa mujibu
wa jarida la JKT, mafunzo hayo yatakuwa ya miezi sita katika Kambi za JKT
Bulombora na Kanembwa mkoani Kigoma, Mlale (Ruvuma), Mafinga (Iringa), Msange
(Tabora) na Oljoro (Arusha).
No comments:
Post a Comment