Licha ya
watahiniwa hao kushindwa kupata alama hizo, zile za ufaulu zimeongezeka kutoka
asilimia 45.40 mwaka 2011 hadi kufikia 64.55 kwa mwaka 2012.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema kuwa watahiniwa 136,946 walioshindwa
kupata alama 30 na wengine 23 walioonekana kudanganya watalazimika kukariri
kidato cha pili mwaka huu.
Mulugo alisema
kuwa watahiniwa 249,325 wataendelea na masomo ya kidato cha tatu.
“Ni vema
ikaeleweka kuwa kukariri kidato sio adhabu bali ni kutoa fursa nyingine kwa
wanafunzi hao kuweza kupata maarifa, stadi na ujuzi wa elimu ya sekondari
kidato cha kwanza na pili kwa kiwango kizuri,” alisema.
Ufaulu wa
watahiniwa.
Kwa ipande
wa ufaulu wa watahiniwa Mulugo alisema kuwa watahiniwa 249,325 sawa na asilimia
64.55 walifaulu huku wasichana wakiwa 113,213 na wavulana 136,112 kiwango
kikipanda kwa asilimia 19.15.
“Watahiniwa
waliofaulu kwa kiwango cha A, B na C walikuwa 127,981 sawa na asilimia 33.13 na
waliofaulu kwa kiwango cha D ni 121,344 na alama ya juu ya ufaulu ilikuwa ni
asilimia 92,” alisema.
Shule
zilizofanya vizuri.
![]() |
Waziri Mulugo |
Mulugo
alizitaja shule za serikali kumi zilizoongoza ni Mzumbe, Tabora wavulana,
Ilboru, Kibaha, Iyunga, Msalato, Malangali, Ifunda Ufundi, Samora Machel na
Kilakala.
Kwa upande
wa shule zisizo za serikali, Mulugo alizitaja kuwa ni Kaizerege, Marian
wavulana, St Francis, Don Bosco, Bethel SABS, Marian wasichana, Don Bosco
Moshi, Cannosa, St Joseph Iterambogo na Carmel.
Shule
zilizofanya vibaya.
Kwa upande
wa shule za serikali zilizofanya vibaya ni Mihambwe, Dinduma, Kiromba, Marambo,
Mbembaleo, Kinjumbi, Litipu, Luagala, Miguruwe na Napacho ambazo zote ni kutoka
mikoa ya kusini – Mtwara na Lindi.
Kwa upande
wa shule zisizo za serikali ni Mfuru, Pwani, Doreta, Kigurunyembe, Ruruma,
At-taaun, Jabal hira, Mkono wa Mara, Kilepile na Kiuma.
Wanafunzi
waliofanya vizuri.
Waziri Mulugo
aliwataja wanafunzi walioongoza katika mtihani huo na shule wanazotoka katika
mabano kuwa ni Magreth Kakoko (St Francis) Queen Masiko (St Francis), Lukundo
Manase (Kaizerege), Frank Nyamtarila (Kaizerege), Grace Msovella (St Francis),
Harieth Makireye (St Francis) Robinnancy Mtitu (St Francis), Humrath Lusheke
(St Francis), Mukhsin Hamza (Kaizerege) na Anastazia Kabelinde (Kaizerege).
Walimu shule
za mijini.
Katika hatua
nyingine, Mulugo alisema kuwa kuanzia mwaka huu hakuna mwalimu atakayepangwa
shule za mjini.
Hatua hiyo imetokana
na ukosefu wa walimu ulioko vijijini na tabia ya walimu wengi kupenda kuishi
mijini.
![]() |
Waziri Mulugo |
Akizungumza
na viongozi wa kanda mbalimbali kutoka Jumuia ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
(Tahliso), Mulugo alisema kuwa mwalimu yeyote ambaye hataripoti katika kituo
chake cha kazi ndani ya wiki mbili atakuwa amejipotezea ajira yake mwenyewe.
Akitoa
nasaha kwa viongozi hao wa Tahliso, Mulugo aliwataka kuachana na tabia ya
kuingiza siasa katika mambo ya elimu kwani husababisha migogoro.
Mulugo
alisema kuwa zinapotokea changamoto zozote vyuoni, ni vyema wanafunzi kukubali
kukaa meza moja ya mazungumzo badala ya kusisitiza migomo na maandamano ya
yasiyoleta tija ambayo huaribu mfumo.
Naye
mwenyekiti wa Tahliso, Amn Chakushemeire, aliwataka wanafunzi wa vyuo vyote
kuacha kutumika na wanasiasa ikiwemo kuondoa chuki za itikadi za vyama vya
siasa ndani ya vyuo vyao.
No comments:
Post a Comment