![]() |
Mbegu za maboga husaidia
kuongeza mbegu za uzazi.
|
Madaktari wengi wameripoti juu ya kuwepo kwa ongezeko
la wagonjwa wengi wa kiume ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya upungufu wa
nguvu za kiume.
Mwaka jana mwishoni gazeti la The Independent llilopo nchini
Uingereza liliripoti kuwa hali ya afya
ya viungo vya uzazi hususani kwa wanaume ilishuka kwa kiwango kikubwa na hiyo
ilitokana na utafiti uliofanywa duniani juu ya ubora wa mbegu za kiume.
![]() |
Nanasi. |
Utafiti huo ulionyesha kuwa
katika miaka ya 1989 hadi 2005 ulionyesha
kuwa kati ya wanaume 26,000 waliofanyiwa uchunguzi robo tatu yake walionekana
kuwa na uwezekano mkubwa wa kushindwa kuzaa.
Mwaka 1989 na
2005, kwa mujibu wa gazeti moja la Uingereza lilisema kwamba “Wanaume 26,000 wanakabiliwa na tatizo hilo
la upungufu wa mbegu za kiume.’’
Utafiti huo uliendelea
kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na
matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa
wanaume wengi duniani.
Miongoni mwa sababu ambazo
zimekuwa zikisababisha nguvu hizo kuporomoka ni pamoja na kuvaaji wa nguo za
ndani ambazo zinabana, pia wataalamu
walieleza kuwa ufumbuzi juu ya sababu maalumu ya nguvu hizo kushuka bado
haujapatikana.
Baadhi ya waandishi nchini
Kenya hususan katika gazeti la Daily
Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo
hilo lipo nchini humo.
Utafiti huo ulifanywa na
daktari mmoja maarufu katika Hospitali ya Royal Garden nchini humo
aliyejulikana kwa jina la Solomon Wasike
ambaye alisema kuwa wiki mbili zilizopita alipata mgonjwa mwenye tatizo kama
hilo.
Aliongeza kuwa mwanamume huyo
alikuwa na umri wa mika 28 alikuwa amefika katika kliniki yake kwa ajili ya
kupima juu ya uwezo wake wa kuzaa.
![]() |
Matunda husaidia
kuongeza mbegu za uzazi.
|
Hali hiyo ilikuja baada ya
kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo
alishindwa kupata mimba.
Daktari Wasike alisema kuwa
baada ya maelezo hayo aliamua kuchukua
mbegu zake mwanaume huyo kwa ajili ya
vipimo aliongeza kuwa majibu yake yalikuwa na utata kwa kuwa yalionyesha kuwa
mtu huyo alikuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha mbegu hali ambayo iliyosababisha
mke wake kutopata mimba.
Wasike alisema kuwa hali hiyo
imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika kliniki hiyo kuwa na wagonjwa wengi wa
kiume wenye matatizo katika afya ya uzazi.
“Kinachotusumbua ni kwamba
vijana wengi wanaokuja katika hospitali
hii wamekuwa na matatizo sawa katika mbegu za kiume na jambo hili
linazidi kusikitisha kwa kuwa asilimia kubwa ya watu wanaokuja ni vijana.
![]() |
Nanasi. |
Aliongeza kuwa hali hiyo
inafanya tuamini kuwa licha ya wengine kuwa na matatizo hayo tangu kuzaliwa
lakini asilimia kubwa ya vijana wanapatwa na tatizo hilo kwa sababu ya hali ya maisha wanayopitia pamoja na mazingira
wanayoishi.
Hata hivyo takwimu za kitaifa
bado hazijafanywa juu ya tatizo licha ya
kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya wanaume kutoka katika katika hospitali
mbalimbali.
Chanzo:Mwananchi.
No comments:
Post a Comment