Azam FC na Miaka 49 ya kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuichapa Tusker ya Kenya Bao 2-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 13, 2013

Azam FC na Miaka 49 ya kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuichapa Tusker ya Kenya Bao 2-1.

Azam FC
Wana Lamba lamba Azam FC, wamefanikiwa kulitwaa kombe la  Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuichapa Tusker ya Kenya Bao 2-1 katika mchezo uliochezwa Dakika 120 baada ya kwenda sare 1-1 katika Dakika 90.




Mbali ya kutwaa Kombe, Azam FC pia walizawadiwa Shilingi Milioni 10 kama Washindi na Tusker kupewa Milioni 5 kama Washindi wa Pili.



Tusker FC
Tusker ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Jesse Were katika Dakika ya 60 na Azam FC kusawazisha kwa Penati ya Dakika ya 72 iliyotolewa kufuatia Luke Ochieng kuushika mpira na Atudo kufunga Penati hiyo.



Bao hizo zilidumu hadi Dakika 90 kumalizika na ndipo zikaongezwa Dakika 30 za Nyongeza na Gaudence Mwaikimba kufunga Bao la Pili na la ushindi, Dakika ya Pili tu ya Muda huo wa Nyongeza.




ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI



Shujaa Mwaikimba baada ya kufunga

bao la kwa Azam FC ushindi usiku huu.
2003   Mtibwa Sugar
2004   Yanga SC
2005   Yanga SC
2006   Simba SC
2007   Yanga SC
2008   Simba SC
2009   Miembeni FC
2010   Mtibwa Sugar
2011   Simba SC
2012   Azam FC
2013   Azam FC 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad