Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa Maandamano ya Wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) Wizara ya Mambo ya ndani na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 15, 2013

Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa Maandamano ya Wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) Wizara ya Mambo ya ndani na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.


Wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia jana(Januari 14,mwaka huu) majira ya saa nne na nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.



 Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa  hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.



Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.


"Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo" Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.


Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na ikielekea Kigamboni.


Wakajazana kupita kiasi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad