Yaya Toure awabwaga Didier Drogba na Alexander Song katika Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya pili Mfululizo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 21, 2012

Yaya Toure awabwaga Didier Drogba na Alexander Song katika Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya pili Mfululizo.


Yaya Toure  , Didier Drogba

na Alexander Song.
Kiungo wa Ivory Coast  na Manchester City Yaya Toure ametajwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya pili mfululizo usiku wa Alhamisi, akimshinda mmpizani wake wa karibu Didier Drogba .


Kiungo huyo mwenye miaka 29 ambaye katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, alichangia kwa kiasi kikubwa kuisadia Ivory Coast kucheza fainali ya AFCON 2012 pai alikuwa ndio mhimili wa Manchester City mpaka walipochukua ubingwa wa England mwezi June mwaka huu.


Pia alikuwa mmoja wa wafungaji katika mechi ya ushindi wa kombe la hisani dhidi ya Chelsea ambapo City walishinda kwa 3-2 - huku akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya taifa kufuzu michuano ya AFCON 2013.



Didier Drogba alishika nafasi ya pili, huku kiungo wa Barcelona Alexander Song akikamata nafasi ya 3 katika tuzo hizo zilizotolewa mjini Accra usiku wa kuamkia leo.



Mohamed Aboutrika alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara, huku timu yake ya Al Ahly ikichaguliwa kuwa timu bora kwa upande wa vilabu wakati mabingwa wa Afrika kitaifa Zambia wakichaguliwa timu bora ya taifa. 


Tuzo zilikuwa kama ifuatavyo .


CAF AWARDS.



Player of the Year - Yaya Toure 


African based Player of the Year - Mohammed Aboutrika


Women's Footballer of the Year - Genoveva Anonma (Equatorial Guinea)


National team of the Year – Zambia


Coach of the Year - Herve Renard (Zambia)


Club of the Year - Al Ahly


Legends Award: Mahmoud El Gohary (Egypt) and Rigobert Song (Cameroon)


National Women's Team of the Year - Equatorial Guinea


Fair Play Award - Gabon national team supporters 


Most Promising talent of the Year - Mohamed Salah (Egypt and FC Basel)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad