![]() |
Dkt. Shukuru Kawambwa
(kushoto)
|
Taarifa hiyo
inaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 560,706 kati ya 865,534 waliofanya mtihani
wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za
serikali, ambapo idadi hiyo ni sawa na
asilimia 64.78 ya wanafunzi waliofanya mtihani.
Aidha kati
ya wanafunzi waliochaguliwa wasichana ni 281,460 sawa na asilimia 50.20 na
wavulana ni 279,246 sawa na asilimia 49.80.
Pia takwimu
zinaonyesha waliofutiwa matokeo kutokana na vitendo vya udanganyifu katika
mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2012 imepungua sana, kwani ni watahiniwa
293 tu ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliofutiwa matokeo mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment