Mahakama ya Rufaa imemrejeshea Ubunge aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Bw Godbless Lema baada ya kushinda rufaa yake ya kupinga hukumu, iliyomvua ubunge. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 21, 2012

Mahakama ya Rufaa imemrejeshea Ubunge aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Bw Godbless Lema baada ya kushinda rufaa yake ya kupinga hukumu, iliyomvua ubunge.


 Lema,Mbowe na Nassari katika

 Mahakama ya rufaa Tanzania

 jijini Dar es salaam




 Lema akianza kutoa hotuba fupi

 baada ya kutoka mahakamani.

kulia ni Mbunge Joshua Nassari.


Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema(CHADEMA) ameshinda rufaa yake katika mahakama ya Rufaa jijini Dar es salaam na kurejea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia jimbo la Arusha mjini.

 

Wafuasi wa chama cha CHADEMA wamepita katika mitaa ya Posta asubuhi hii huku wakishangilia na kuonyesha vidole viwili juu huku wakiimba Lema …..Lema.




Hukumu imeangalia haswa swala la Locus Stand ya kama waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo.



Imeangaliwa kwa kina na kuonekana kuwa kadiri ya pingamizi ya mawakili wa Lema Kimomogoro na Tundu Lissu, waliofungua shitaka dhidi ya Lema hawakuwa na locus stand ya kufanya hivyo.



Kwa hiyo mengine yote yanakuwa null and void. 



Hukumu haikuchukua hata nusu saa,Hivyo basi Lema ni mbunge halali wa Arusha mjini tangia leo.







Mawakili wakiwa kwenye viti vyao.

Hawa ndiyo waliokuwa wamefungua kesi dhidi ya Lema wakiwa Mahakamani .

Vitalisi Kimomogoro,wakili wa Lema.huyu ndiye amekuwa na kesi hii tangu kuanza kwake.


Aidha Mahakama ya Rufaa imemrejeshea ubunge  Godbless Lema baada ya kushinda rufaa yake ya kupinga hukumu iliyomvua ubunge .


Hukumu hiyo  inatokana na rufaa iliyokatwa na Lema, ambaye anapinga hukumu iliyotolewa Aprili 15, mwaka huu na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ambayo ilitengua ubunge wake.



Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Nathalia Kimaro  limesema hukumu ya kutengua matokeo ya ubunge wa  Lema  ilikuwa na makosa hivyo Mbunge huyo ataendelea na wadhifa wake .


Tundu Lisu mtetezi wa Lema aliingia baada ya kesi kufika mahakama ya rufaa…….ameshangiliwa sana.




Hapa Lema akiwa na Kilewo wakati wa maandamano ya kutoka mahakamani kuelekea makao makuu ya CHADEMA.



 Askari Polisi  wakisindikiza msafara wa wafuasi wa CHADEMA –Dar es Salaam.


Awali mahakama kuu kanda ya Arusha, ilitengua ubunge wa Bw Lema baada ya kuridhika kuwa, alitumia lugha ya matusi dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, katika uchaguzi wa mwaka 2010  Dr Batilda Burian. 




Baada ya Godbless Lema kushinda ubunge wake jijini dar es salam huko arusha ni furaha katika makundi mbalimbali,Vijana wamesimama katika makundi madogo madogo na wale waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wakipiga hono mji mzima ambapo watu maweacha kufanya shugulu zao na kujadili ushindi wa mbunge wa jimbo hilo la arusha mjini.hali ni shwari kabisa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad