Tairi la gari |
Jeshi la
Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya marehemu Hussein
Ramadhan, ‘Sharo Milionea’ vilivyoibwa na watu wasiojulikana, muda mfupi baada
ya msanii huyo wa filamu na muziki nchini kupata ajali katika Kijiji cha Songa
Kibaoni, wilayani Muheza na kufariki dunia papo hapo.
Akizungumza
na waandishi wa habari , Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Costantine Massawe
alisema Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata begi la nguo, simu ya mkononi
aina ya blackberry, betri ya gari, redio, tairi la gari na saa ya mkononi ya
marehemu.
Alitaja vitu
vingine vilivyopatikana kuwa ni nguo ambazo marehemu alivuliwa baada ya kupata
ajali, ambazo ni fulana na suruali ya jeans.
Alisema
kuwa,vitu hivyo vilipatikana baada ya wakazi wa kijiji ilipotokea ajali hiyo
kuvisalimisha vitu hivyo kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Songa kibaoni, Abdi
Zawadi ambaye alitoa taarifa polisi kwa ajili ya utambuzi na taratibu nyingine,” .
Begi la nguo, simu ya mkononi aina ya blackberry, betri ya gari, redio |
Kamanda
Massawe alisema baadhi ya vitu hivyo vilikamatwa nje ya wilaya ya Muheza katika
gereji na kwenye nyumba za watu.
Kamanda
alifahamisha zaidi kuwa, hadi sasa watu kadhaa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa
kuhusika na tukio hilo lakini hakutaja idadi yao kwa kuwa vitu vingine
havijapatikana.
Gari
aliyokuwa akiendesha Marehemu Sharomilionea baada ya kuacha njia na
kupinduka
|
No comments:
Post a Comment