Fans wa Kilimanjaro Stars |
Timu
ya Tanzania Bara imefanikiwa kuingia
Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya
kuilaza Timu ya Rwanda mabao 2 - 0 kwenye Uwanja wa Lugogo mjini Kampala Uganda.
Hadi
mapumziko Kilimanjaro Stars walikuwa
mbele kwa bao 1 - 0 lililotiwa kimiani na kiungo Amri Kiemba, dakika mya 33
akiunganisha pasi ya Mwinyi Kazimoto aliyewapunguza wachezaji wawili wa Rwanda
kabla ya kutoa pasi maridadi.
Kipindi
cha pili Kilimanjaro Stars walirudi
vizuri tena na kuendelea kucheza kwa kuonana na kufanikiwa kupata bao la pili
53 baada ya John Bocco kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Jean Claude Ndoli
kufuatia shuti kali la Mwinyi Kazimoto kutoka nje ya eneo la hatari.
Kwa
ushindi huo Kilimanjaro Stars sasa inasubiri mshindi kati ya Uganda na
Ethiopia kesho watakapo kutana naye kwenye hatua ya Nusu Fainali.
Zanziba Heros |
Nao
Zanziba Heros imeingia hatua ya Nusu Fainali ya Kombe hilo la CECAFA Tusker Challenge baada ya
kuifunga Burundi kwa penalti 5 - 4 kwenye Uwanja huo huo wa Lugogo mjini Kampala, Uganda kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya
dakika 90.
Kwa
matokeo hayo, Zanzibar sasa itacheza na mshindi kati ya Kenya na Malawi katika
Nusu Fainali.
Shujaa
wa Zanzibar alikuwa ni Abdallah Othman
aliyefunga penalti ya mwisho, baada ya kipa Mwadini Ally kupangua penalti ya
Abdul Fiston wa Burundi.
Aidha
manahodha wa timu zote, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar na Suleiman
Ndikumana wa Burundin walipoteza penalti zao leo.
Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichopambana na Burundi
katika mchezo wa Robo Fainali ya Pili ya michuano ya Cecafa Challenge
uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda.
|
No comments:
Post a Comment