Akiongea na
wananchi katika msiba huo Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Bw Philip Kalangi
amesema nchi inaongozwa na utawala wa sheria hivyo Serikali haitakubali watu
kujichukulia sheria.
Amesema Polisi wanajukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao na kwamba polisi na
raia watakaobainika kuhusika na tukio hilo watachukuliwa hatua stahiki.
Mwananchi
aliyeuawa na Polisi na kuzikwa jana ni Said Nkonikoni mkazi wa Mugoma na askari Polisi waliouawa na wananchi wenye hasira, Koplo Pascal na Konstebo Alex wa
Kikosi cha Usalama Barabarani ambao miili yao imeagwa jana na kupelekwa mikoa
ya Mwanza na Morogoro kwa maziko.
Habari:Radio Kwizera/www.radiokwizera.com
No comments:
Post a Comment