Chelsea yashindwa na Corinthians 1- 0 kutoka Brazil na kushinda kombe la klabu Bingwa Duniani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 16, 2012

Chelsea yashindwa na Corinthians 1- 0 kutoka Brazil na kushinda kombe la klabu Bingwa Duniani.



Petr Cech-Chelsea.
Klabu ya Corinthians has become only the second team ever to win the Club World Cup twice after defeating Chelsea 1-0 in the final in Yokohama.


Aidha matokeo hayo yamemfanya kocha Rafael Benitez kushindwa kutwaa Taji lake la kwanza kama Meneja wa Chelsea baada ya bao pekee la Mechi hiyo lililofungwa na Paolo Guerrero katika Dakika ya 69 kwa kichwa akiwa katikati ya Wachezaji watatu wa Chelsea.



Chelsea wangeweza kulazimisha Mechi iende Dakika 30 za nyongeza lakini Fernando Torres akiwa pekee na Kipa Cassio alimpelekea moja kwa moja Kipa huyo.



Nae Gary Cahill  ambae pia alikosa nafasi ya wazi, alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kuvaana na Emerson katika tukio ambalo mpira ulikuwa haupo kwao.



Corinthians
 Katika Dakika za Majeruhi, Torres alitumbukiza mpira wavuni lakini Bao hilo lilikataliwa kwa kuwa alikuwa Offsaidi.

 

Katika mchezo wa  kutafuta Mshindi wa 3 iliyochezwa leo kabla ya Fainali, Monterrey waliibuka washindi kwa Bao 2-0 walipoifunga Al Ahly ya Misri.




MABINGWA WALIOPITA.

-2000 - Corinthians

-2005 - Sao Paulo

-2006 - Internacional

-2007 - AC Milan

-2008 - Manchester United

-2009 - Barcelona

-2010 - Inter Milan


-2011 - Barcelona

-2012 - Sport Club Corinthians Paulista



KLABU BINGWA DUNIANI 2012-TIMU ZITAKAZOSHIRIKI.
 


Corinthians1-0 Chelsea
Chelsea-BINGWA ULAYA

Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI

Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI

Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA

Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia

Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika

Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad