Tanzania yazindua chanjo mpya za “PVC 13 na Rotarix” kukinga watoto dhidi ya Nimonia na magonjwa ya kuhara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 08, 2012

Tanzania yazindua chanjo mpya za “PVC 13 na Rotarix” kukinga watoto dhidi ya Nimonia na magonjwa ya kuhara.


Mama Salma Kikwete akihutubia katika uzinduzi wa chanjo mpya katika kituo cha afya Buguruni ambapo amesema Idadi ya magonjwa yanayokingwa kwa chanjo imeendelea kuongezeka kutoka manne hadi tisa kufikia 2009 na kuwa chanjo inayozinduliwa itafanya maradhi yanayokingwa kwa chanjo kufikia 11.



Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akisoma hotuba yake.




Baadhi ya Kinamama

na watoto wao waliojitokeza

katika uzinduzi wa Chanjo hizo.

Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo imezindua chanjo mpya zinazolenga kukinga watoto dhidi ya nimonia na magonjwa ya kuhara yanayo sababishwa na kirusi cha Rotavirus.
 

Akizindua chanjo hiyo leo Mke wa rais Mama Salma Kikwete amesema kirusi cha Rotavirus kinachangia asilimia 18 ya vifo vya watoto vinavyotokana na kuharisha.


Amesema kuongezeka kwa chanjo hizi hapa nchini kutapunguza vifo vya watoto vitokanavyo na maradhi haya ili kufikia lengo la mileni namba 4 ifikapo 2015.


Aidha Mama Salma ametoa rai kwa wananchi kuendeleza juhudi mbalimbali za kuboresha afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa nyakati muhimu hususan kabla ya kula au kuandaa chakula, pia baada ya kujisaidia.




Mama Salma Kikwete akitoa chanjo kwa mmoja wa watoto kuashiria uzinduzi wa chanjo mpya za “PVC 13 na Rotarix” kukinga watoto dhidi ya Nimonia na magonjwa ya kuhara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad