UEFA CHAMPIONS LEAGUE |
CRISTIANO
Ronaldo atarejea Manchester United akiwa na mabingwa mara tisa Real Madrid
katika mechi ya hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya huku Lionel
Messi wa Barcelona akiwakabili AC Milan ya Italia.
Bayern
Munich ambao msimu uliopita walifungwa
katika fainali na Chelsea, watacheza dhidi ya Arsenal wakati Juventus
itaikabili timu ambayo haikutarajiwa kufika hatua hiyo ya Celtic.
Timu
inayotumia pesa nyingi kusajili wachezaji ya Paris St Germain itacheza dhidi ya
Valencia.
Lakini
ratiba ya miamba wawili wa Hispania ndiyo iliyovutia tukio hilo la leo katika
makao makuu ya UEFA na wote wawili walipangiwa timu ambazo ni mabingwa wa
zamani wa Ulaya.
Manchester United |
Lakini
Ronaldo atakuwa na hamu kubwa ya kuiinua timu yake ya Madrid dhidi ya klabu yake ya
zamani aliyoiongoza kutwaa ubingwa huo wa Ulaya mwaka 2008 na ambayo ilimsaidia
kuwa mshambuliaji wa kiwango cha dunia na pia katika uwanja wa Old Trafford Jijini London
Uingereza kwa mara ya kwanza tangu ahame
hapo na kwenda Real Madrid Mwezi Juni Mwaka 2009 kwa Dau la Pauni Milioni 80.
Kocha wa
Real, Jose Mourinho, ambaye aliwahi kuifundisha Chelsea, pia atakumbana na
hasimu wake wa zamani Alex Ferguson.
"Ninaamini
itakuwa mechi 'spesho' kwake (Ronaldo)," alisema Emilio Butragueno,
mkurugenzi wa mahusiano wa Real Madrid. "Nadhani mashabiki watakuwa na
furaha kubwa, kubwa sana kwa mechi hii itakayokuwa na mvuto wa aina yake.
"Itakuwa
kitu kizuri kwa kila mmoja."
Barcelona
Tito Vilanova
|
Messi
amefunga magoli 90 mwaka 2012 ameiongoza Barcelona kukaa kileleni mwa msimamo
wa La Liga kwa tofauti ya pointi tisa wakati Milan wako pointi 14 nyuma ya
vinara Juventus katika mbio za ubingwa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) na
walimaliza wa pili nyuma ya Malaga katika kundi lao.
Makamu wa
rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu aliiambia televisheni ya Hispania ya
Canal Plus: "Milan ni moja ya klabu kubwa za Ulaya na ni timu ambayo
inaheshima kubwa.
"Hawafanyi
vyema hivi sasa katika ligi yao lakini wana wachezaji wazuri. Hawako katika
kiwango chao cha juu kwa sasa lakini soka hubadilika siku moja kwenda
nyingine."
Katika mechi
nyingine, Galatasaray watacheza dhidi ya Schalke 04, Shakhtar Donetsk
watawakabili Dortmund na Porto watawavaa Malaga.
Ratiba ya Ligi ya 16-Bora Klabu Bingwa Ulaya iliyopangwa mjini Nyon Nchini Uswisi:
Ratiba ya Ligi ya 16-Bora Klabu Bingwa Ulaya iliyopangwa mjini Nyon Nchini Uswisi:
Galatasaray v Schalke 04
Celtic v Juventus
Arsenal v Bayern Munich
Shakhtar
Donetsk v Borussia Dortmund
AC
Milan v FC Barcelona
Real
Madrid v Manchester
United
Valencia v Paris St Germain
Porto v Malaga
*Washindi wa
pili wa hatua ya makundi wanaanzia nyumbani.
* Mechi za
kwanza zitachezwa Feb 12/13 na 19/20, za marudiano zitapigwa Machi 5/6 na 12/13.
EUROPA LEAGUE LAST 32 DRAW |
BATE Borisov | VS | Fenerbahce |
Inter | VS | CFR Cluj |
Levante | VS | Olympiakos |
Zenit St Petersburg | VS | Liverpool |
Dynamo Kiev | VS | Bordeaux |
Bayer Leverkusen | VS | Benfica |
Newcastle United | VS | Metalist Kharkiv |
Stuttgart | VS | Genk |
Atletico Madrid | VS | Rubin Kazan |
Ajax | VS | Steaua Bucharest |
Basel | VS | Dnipro |
Anzhi | VS | Hannover |
Sparta Prague | VS | Chelsea |
Borussia Monchengladbach | VS | Lazio |
Tottenham | VS | Olympique Lyonnais |
Napoli | VS | Viktoria Plzen |
No comments:
Post a Comment