Santi Cazorla amepiga hetitriki na kuisaidia klabu yake ya Arsenal kupata ushindi mnono na hivyo kushika nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu soka nchini Uingereza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 18, 2012

Santi Cazorla amepiga hetitriki na kuisaidia klabu yake ya Arsenal kupata ushindi mnono na hivyo kushika nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu soka nchini Uingereza.


Santi Cazorla
Mchezaji wa Hispaina Santi Cazorla amepiga hetitriki na kuisaidia klabu yake ya Arsenal kupata ushindi mnono na hivyo kushika  nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu soka nchini  Uingereza baada ya kuwatandika Reading  bao 5-2 wakiwa kwao Uwanja wa Madejski Jumatatu Usiku.

 

Arsenal walitangulia mbele kwa bao 4-0  baada ya Lukas Podolski kufungua goli moja na Santi Cazorla kupiga  ma3 lakini Reading wakapata Bao mbili kupitia Adam Le Fondre na Jimmy Kebe na kuifanya gemu iwe 4-2. 



Hii ilikuwa ni Mechi muhimu mno kwa Arsenal kushinda hasa baada ya Wiki iliyopita kubwagwa nje ya CAPITAL ONE CUP na Timu ya Daraja la chini Bradford na kuleta mfarakano kwa Wadau wao ambapo  Mara ya mwisho Timu hizi kucheza ilikuwa Uwanja huu huu wa Madejski na Arsenal kushinda Bao 7-5 kwenye Mechi ya CAPITAL ONE CUP. 



MSIMAMO.




1 Man United Mechi 17 Pointi 42

2 Man City Mechi 17 Pointi 36

3 Chelsea Mechi 16 Pointi 29 [Tofauti ya Magoli 11]

4 Tottenham Mechi 17 Pointi 29 [Tofauti ya Magoli 5]


5 Arsenal Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 13]

6 Everton Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 7]

7 WBA Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 3]

8 Norwich Mechi 17 Pointi 25




RATIBA MECHI ZIJAZO:

Jumamosi 22 Desemba 2012



[SAA 9 Dak 45 Mchana]


Wigan v Arsenal

[SAA 12 Jioni]

Man City v Reading

Newcastle v QPR

Southampton v Sunderland

Tottenham v Stoke

West Brom v Norwich

West Ham v Everton

[SAA 2 na Nusu Usiku]

Liverpool v Fulham



Jumapili 23 Desemba 2012

[SAA 10 na Nusu Jioni]

Swansea v Man United

[SAA 1 Usiku]

Chelsea v Aston Villa
 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad