Rais Zuma wa Afrika Kusini achaguliwa tena kukiongoza chama cha ANC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 18, 2012

Rais Zuma wa Afrika Kusini achaguliwa tena kukiongoza chama cha ANC.

Rais  Jacob Zuma
Rais  Jacob Zuma wa  Afrika  kusini  amechaguliwa tena kukiongoza chama  tawala  cha  African National Congress (ANC).


Bw.  Zuma  ameshinda  kwa  karibu  kura 3,000, wakati  Makamu wake aliyekuwa pia akiwania nafasi hiyo Kgalema Montlante amepata  kura  chini  ya  1,000  katika uchaguzi  wa  uongozi  wa  chama  hicho  uliofanyika  leo.



Upigaji  kura  ulianza  asubuhi  ya  leo  katika  mkutano  wa ANC  wa  Mangaung, uliofanyika  katika  mji  ambao  pia unafahamika  kama  Bloemfontein.



Takriban wajumbe  4,000  wamepiga  kura  katika kinyang’anyiro  hicho  cha  uongozi  wa  juu  wa  chama cha  ANC.




Wajumbe wa chama cha ANC

Bwana Motlanthe sasa amepoteza nafasi yake ya naibu kiongozi wa chama hicho na mahala pake pamechukuliwa na mfanyabiashara maarufu na mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi Cyril Ramaphosa, ambaye sasa atakuwa makamu wa rais wa Afrika Kusini. Mshindi wa nafasi hiyo ndiye atakayekuwa na nafasi ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2014.

 

Chama cha ANC kimeshika hatamu nchini Africa Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.



Polisi nchini humo, hapo jana waliwatia mbaroni watu wanne baada ya taarifa kuzagaa kwamba walikuwa na mpango wa kulipuwa ukumbi unaotumiwa na wajumbe hao wa chama cha ANC.



Baada ya uchaguzi huo kucheleweshwa kwa masaa kadhaa, zoezi la kupiga kura lilianza saa sita usiku na kukamilika majira ya saa moja asubuhi kwa saa za Afrika Kusini.



Wajumbe hao walioonekana wamechoka huku wakijifunika mablanketi walionyesha vidole vyao vikiwa na alama ya wino.



Wajumbe hao wamekuwa wakipiga kura kwa ajili ya nafasi ya uongozi wa juu wa chama hicho.



Rais Zuma
Wafuasi wa rais Zuma, tayari wanaendelea kusheherekea, kufuatia ushindi huo mkubwa.



Rais Zuma analaumiwa kwa kushindwa kupunguza umaskini au kutatua tatizo la ufisadi ndani ya chama cha ANC na serikali, wakati mwezi wa nane mwaka huu watu walishangazwa na jinsi polisi walivyowapiga risasi na kuwauwa wachimba madini 34 ambao walikuwa wamegoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad