Barnaba Boy asema ni upumbavu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kushoot video za muziki wao kutoka maeneo ya nje ya nchi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 19, 2012

Barnaba Boy asema ni upumbavu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kushoot video za muziki wao kutoka maeneo ya nje ya nchi.

Siku chache baada ya kukamilisha kushoot video ya  ngoma  yake mpya ya 'Sorry' nyota kutoka nyumba ya vipaji nchini (THT) Barnaba Boy amesema ni upumbavu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kushoot video za muziki wao kutoka maeneo ya nje ya nchi.


 
Katika mahojiano maalum aliyoyafanya na teentz.com mapema leo Barnaba amesema kuwa, wakati mwingine inaweza isiwe jambo baya lakini  kwake anaona ni upumbavu kufanya hivyo wakati nchi hii ya Tanzania  imebarikiwa kuwa na vitu kibao vya kuvutia ambavyo vinaweza kupamba video ya wimbo husika.



"Hivi sasa naona watu wengi wanakimbilia kufanya video nje, si mbaya lakini binafsi siwezi fanya jambo hilo kwa kuwa naipenda nchi yangu na natamani kuendelea kuitangaza kila siku soo nahisi ni jambo bora kufanya video zangu hapa,bongo kwa kutumia warembo wa hapa na huo ndiyo uamuzi wangu ambao nahisi sitaubadilisha kamwe" alisema.




 

Barnaba - (Am sorry) video teaser. 

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad