Lulu |
Kutokana na
mabadiliko hayo, Lulu ameepuka adhabu hiyo kwani hata kama atapatikana na
hatia, adhabu yake ni kifungo cha maisha au kuachiwa huru.
Hii
inatokana na kifungu cha 196 cha kanuni za adhabu ya kosa la kuua bila
kukusudia, ambapo anayepatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha,
miaka kadhaa au kuachiwa huru.
Hata hivyo,
baadhi ya wanasheria waliliambia gazeti hili kwamba uzoefu wa adhabu nyingi za
kuua pasipo kukusudia zilizowahi kutolewa nchini, ni kati ya miaka 15 na
wengine waliachiwa huru.
Lulu
alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Aprili 11, mwaka huu akikabiliwa
na tuhuma za kumuua Kanumba Aprili 7, 2012.
Alikuwa
akidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa
Makosa ya Jinai (CPA), shtaka ambalo mshtakiwa anayepatikana na hatia adhabu
yake ni kunyongwa hadi kufa.
Hata hivyo,
jana upande wa mashtaka ulieleza mahakamani kuwa kwa sasa imebadilisha mashtaka
kutoka kuua kwa kukusudia na kuwa kuua bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha
195 cha CP.
Mshtakiwa
huyo alitarajiwa kusomewa mashtaka hayo mapya jana pamoja na maelezo yote ya
kesi, ambapo angesomewa ushahidi wa mashahidi wote pamoja na vielelezo muhimu
katika kesi hiyo.
Hata hivyo,
hatua hiyo ilikwama kutokana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka
anayeiendesha kesi hiyo kutokuwapo mahakamani na badala yake aliwakilishwa na
Wakili wa Serikali, Ofmedy Mtenga.
“Upelelezi
wa shauri lako umeshakamilika na tungeweza kukusomea comital (maelezo ya kesi)
leo, lakini kwa kuwa waendesha mashtaka hawapo basi tunaliahirisha mpaka tarehe
nyingine.”, alisema Hakimu Mkazi Agustina Mmbando, anayesikiliza kesi hiyo
katika hatua hiyo ya awali.
Taarifa hizo
za kukamilika kwa ushahidi wa kesi hiyo zilipokewa kwa furaha na shangwe na
msanii huyo, kiasi kwamba alishindwa kujizuia kuonyesha furaha yake.
Wakili wake
Peter Kibatala aliiomba mahakama itoe ahirisho fupi hadi Ijumaa kwa ajili ya
mshtakiwa kusomewa mashtaka haya mapya pamoja na maelezo ya awali.
Hakimu
Mmbando alikubaliana na ombi hilo la Wakili Kibatala na akaahirisha kesi hiyo
hadi Ijumaa.
Source:Mwananchi.
No comments:
Post a Comment