Mrisho Ngasa |
El-Mereik
wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho
Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha
mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo
vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.
Kuuzwa kwa
Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya
Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza
Mrisho Ngasa.
Wakati Azam
FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka
lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi
milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye
kufikia dau hilo waweze kumuuza.
Mrisho Ngasa |
Mengi yalisemwa
juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC
uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh kufikia dau la
kumnunua Mrisho Ngasa.
Mrisho
Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda
nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki na kati baada ya TP Mazembe.
Azam FC
inamuuza Mrisho Ngasa kwa kuzingatia umuhimu wa maendeleo ya mchezaji mwenyewe
kimpira na kwa kipato, pia kwa kuzingatia kwamba Tanzania inahitaji wachezaji
wengi wanaocheza nje kwenye vilabu vikubwa ili wanaporudi waweze kuisaidia timu
ya Taifa.
Taarifa
zinasema Mrisho Ngassa mwenyewe amepewa
dola 50,000 (sawa na Sh. milioni 79) kwa ajili ya kusaini na atalipwa mshahara
wa dola 4,000 (sawa na Sh. milioni 6.3) kwa mwezi ambako
amesaini mkataba wa miaka miwili
.
Imetolewa na
Utawala.
No comments:
Post a Comment