Mionzi ya simu za mkononi inaweza kuathiri maendeleo ya ubongo wa watoto walioko tumboni mwa mama zao, utafiti umeeleza.Utafiti huo umetaja madhara mengine ya mionzi ya simu za mkononi kuwa ni uharibifu wa manii, mimba, kupungua kwa nguvu za kiume, kupoteza kumbukumbu na kuzaa watoto watukutu.
Pia umeeleza
kuwa matumizi kupita kiasi ya simu hizo, husababisha mtindio wa ubongo na
upungufu wa udadisi kwa watoto tangu udogo wao.
Hata hivyo,
utafiti huo uliofanywa na Shule ya Tiba na Dawa ya Chuo Kikuu cha Yale,
Marekani na kuripotiwa na Gazeti la The Telegraph la Uingereza, umepingwa na
watafiti wengine, wakisema haujakidhi baadhi ya vigezo ili kuuthibitisha.
Kiongozi wa
jopo la utafiti huo, Profesa Hugh Taylor alisema utafiti huo ulioanzia kwa
panya, baadaye ulithibitika kwa binadamu.
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy alisema utafiti huo unaweza kuwa
msaada mkubwa kwa nchi kama Tanzania ambayo hivi sasa ndiyo imechipukia katika
matumizi ya simu za mkononi.
No comments:
Post a Comment