Kesi ya kusababisha madhara kwa kung’ata na kula nyama ya uso wa binadamu inayomkabili Iman Paul mkazi wa Muhange wilayani Kakonko imeendelea katika mahakama ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 24, 2012

Kesi ya kusababisha madhara kwa kung’ata na kula nyama ya uso wa binadamu inayomkabili Iman Paul mkazi wa Muhange wilayani Kakonko imeendelea katika mahakama ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.


Kijana  Susuruka aliyeng’atwa

 na kuliwa nyama ya uso

akiendelea vema

na matibabu yake

katika Hospitali ya

Kibondo –Kigoma.

Kesi ya kusababisha madhara kwa kung’ata na kula nyama ya uso wa binadamu  inayomkabili mkazi wa kijiji cha Muhange wilayani Kakonko imeendelea leo(Desemba 24,2012) katika mahakama ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

 

Mbele ya Hakimu wa wilaya  Erick Marley, mwendesha mashitaka wa Polisi Fadhil Tambale amemtaja mshitakiwa kuwa ni Iman Paul mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa Muhange ya juu wilayani Kakonko .

 

Tambale amesema Novemba 15 mwaka huu mshitakiwa alisababisha madhara kwa kijana aliyetambuliwa kwa jina moja la Susuruka. 




Kijana  Susuruka aliyeng’atwa

 na kuliwa nyama ya uso

akiendelea vema

na matibabu yake

katika Hospitali ya

Kibondo –Kigoma.
Kwa upande wake mshitakiwa Iman Paul amekana shitaka hilo na kupelekwa rumande.



Hakimu wa wilaya ya Kibondo Erick Marley ameahirisha kesi hiyo mpaka Januari,7,2013 ili kutoa nafasi kwa jeshi la Polisi kuendelea na upelelezi wa tukio hilo.         

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad