Hadi sasa tayari wakazi sita wa
kijiji cha Mugoma wilayani Ngara, wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya
Ngara mkoani Kagera wakishitakiwa kwa
mauaji ya Askari wawili na kuchoma moto kituo hicho cha Polisi kata ya Mugoma
wilayani humo.
Kwa mujibu wa waendesha mashitaka wa
Jeshi la Polisi Hamisa Mataka na Tumaini Membi, wamewataja
washitakiwa kuwa ni Method John ambaye ni afisa Mtendaji wa kijiji cha
Mugoma, Suleimu Zuberi, Rashid Ally, Issa Athumani,
Simon Chuma na Aman Maulid.
Washitakiwa hao wanatuhumiwa kuwaua Koplo Paschal na Konstebo
Alexandar, ambao walikuwa waajiriwa wa jeshi la polisi Tanzania,
katika tukio lililotokea Desemba 15 mwaka huu huku Katika shitaka la pili, watu hao
wanashitakiwa kwa kosa la kuchoma moto kituo cha polisi cha Mugoma, na
kusababisha hasara yenye thamani ya zaidi shilingi milioni 68, kutokana na
uharibifu wa mali mbalimbali za jeshi hilo.
Washitakiwa wako rumande hadi January 3 mwaka 2013 kesi hiyo
itapkapotajwa tena.
Picha na :Wiliam Mpanju.
No comments:
Post a Comment